Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ubunge Mbarali: ACT-Wazalendo yamtega Rais Samia
Habari za Siasa

Ubunge Mbarali: ACT-Wazalendo yamtega Rais Samia

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimesema kinashiriki uchaguzi wa marudio wa ubunge katika Jimbo la Mbarali, ili kuipima Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kama inatekeleza azma yake ya mageuzi katika demokrasia ya vyama vya vingi, kwa kuufanya uwe huru na wa haki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado katika hotuba yake ya kufunga kampeni jana tarehe 18 Septemba kwenye Kata ya Rujewa.

“Serikali ya Rais Samia imetoa ahadi ya kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini. Hivi karibuni, kupitia mikutano ya wadau wa demokrasia iliyoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Baraza la Vyama vya Siasa, Serikali imesema ipo tayari kufanya mageuzi ya kisheria ili kuruhusu kushamiri kwa demokrasia. Yote haya hayatakuwa na maana iwapo demokrasia itaendelea kuhujumuwa kwenye chaguzi ndogo” alisema Ado.

Ado alisema “uchaguzi huu wa Mbarali ambao utafanyika na uchaguzi wa marudio kwenye kata sita Nchini ni mtihani kwa Serikali ya Rais Samia, kuwa ipo tayari kusimamia demokrasia kwa vitendo au ni maneno matupu. Iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki, dunia nzima itajua nia ya dhati ya kujenga demokrasia ipo. Iwapo uchaguzi wa Mbarali utavurugwa, dunia nzima itajua ahadi ya demokrasia ni maneno matupu.”

Katika hatua nyingine, Ado Shaibu aliwapongeza viongozi wa kisiasa wilayani Mbarali kwa kuweka pembeni tofauti za kisiasa na kufanya pamoja.

“Mgombea wetu Ndugu Kirufi anaungwa mkono na vyama vingi. Wana Mbarali mmeweka tofauti zenu pembeni ili kuhakikisha mnaipigania ardhi yenu mliyoporwa. Hili ni funzo kwetu wanasiasa wa kitaifa kwamba tunapopigania maslahi mapana kwa Taifa kama vile tunapodai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima vyama vyote tuungane. Bila umoja hakuna ushindi,” alisema Ado.

Uchaguzi huo unafanyika leo tarehe 19 Septemba 2023, ambapo wagombvea kutoka vyama 13 wamepitishwa kugombea katika uchaguzi huo, akiwemo wa ACT-Wazalendo, Modestus Kirufi .

Wengine ni Mary Moses Daudi (UPDP), Fatuma Rashidi Ligania (NLD), Bahati Keneth Ndingo (CCM), Bariki Oswald Mwanyalu (Demokrasia Makini), Hashim Abasi Mdemu (ADC), Mwajuma Noty Mirambo (UMD), na Husseni Hasani Lusewa kutoka Chama cha ADA- TADEA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!