November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Diamond, Zari watamba Tiffah kuvaa joho

Spread the love

 

Msanii wa Bongo fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameonyesha furaha ya kipekee baada ya mwanawe wa kwanza Tiffah Princess kuhitimu kuingia darasa lingine. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Tiffah mwenye umri wa miaka 6 ameingia darasa la kwanza mwaka huu, baada ya kuhitimu kwenye shule moja ya kifahari huko Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tiffah Princess amechapisha ujumbe wa kuonyesha furaha yake hasa ikizingatiwa nchi hiyo imekumbwa na janga la Corona.

“Mwaka 2022 ulianza na sherehe ya kufuzu darasa lingine, kwangu hafla ni ambayo haikufanyika mwaka jana kwa sababu ya idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya Corona… lakini niko hapa sasa. Home girl amehitimu na kuingia darasa la juu,” aliandika Tiffah.

Baada ya kutupia posti hiyo na mashabiki wa Tiffah kumpongeza, Diamond alichapisha picha yake kwenye ukurasa wake wa instagram ikiambatanisha na ujumbe kwamba anajivunia kuwa baba wa mtoto huyo.

Diamond na mpenzi wake wa zamani Zari Hassan wana watoto wawili ambao ni Princess Tiffah na Prince Nillian ambao wote wanaishi na mama yao nchini Afrika kusini.

Mama wa Diamond pia hakubaki nyuma kummiminia mjukuu wake pongezii ambapo alichapisha clip za video akiwa na binti huyo.

error: Content is protected !!