MKUU wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele ametoa tahadhari kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo yalliyokumbwa na mafuriko ya maji yaliyofunguliwa kutoka kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere wahame kwa kuwa bado yanaendelea kufunguliwa. Anaripoti Faki Ubwa, Pwani … (endelea).
Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumapili kwa njia ya simu, Gowele amesema ili kuokoa mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ni lazima maji yapunguzwe yawe katika kiwango kinachohitajika.
“Tumeambiwa tuwe na tahadhari kwa wananchi wanaoishi mabondeni kwani Bwawa la Mwalimu Nyerere linaendelea kufunguliwa ili kuokoa mradi huu.”
Kuhusu taarifa ya kiwango cha maji kitachofunguliwa amesema kitakuwa ni zaidi ya lita milioni 7.
DC Gowele amesita kufafanua zaidi na kusisitiza kuwa hayo ni masuala la kitaam hivyo hawezi kukisia.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Isihaka Mchinjita aliyekwenda Rufiji jana Jumamosi katika eneo lenye maafa, amesema hali ni mbaya na kwamba Serikali onatakiwa itoe taarifa ya maafa kwa umma ili watu Watanzania wajue kinachoendelea.
Mchinjita ambaye pia ni Waziri Mkuu Kivuli wa Baraza la Mawaziri Vivuli la Chama hicho ameitaka Serikali kuwafidia wananchi walioathirika na maafa hayo yaliyosababishwa na kufunguliwa na kwa Bwawa la Mwalimu Nyerere.
Mchinjita wa ACT Wazalendo, unaongea ili usikike kama mpinzani mjinga. Bila bwawa la Nyerere maafa yangezidi. Wananchi walitangaziwa na wametangaziwa. Mabondeni waondoke. Wametangaziwa tena. Siasa zako zingependeza ungeendelea kutangazia na kuwaelisha watu. Haya ni mafuriko yanayadhibitiwa, na mradi bado unaendelea kujengwa.