Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Silaa atoa siku 90 kwa Katibu mkuu ardhi kupima eneo la Olmoti
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Silaa atoa siku 90 kwa Katibu mkuu ardhi kupima eneo la Olmoti

Spread the love

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaaa amemuelekezw Katibu Mkuu wa wizara yake kuhakikisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wamefika eneo la Olmoti linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa Jijini Arusha na kuhakikisha ndani ya kuanzia kesho Juumatatu wanaweka mpango wa upangaji na upimaji wa eneo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).


Waziri Silaa amesema hayo jana Jumamosi wakati wa hafla ya kumkabidhi Mkandarasi eneo la ujenzi wa Uwanja wa Kisasa wa Mpira wa Miguu unaotarajiwa kujengwa eneo  la Olmoti lililopo Jijini Arusha.

Aidha, Waziri Silaa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake kuhakikisha maeneo yote yanayozunguka uwanja huo wa michezo unaotarajiwa kujengwa ni lazima yawe yamepangwa na kupimwa ili kupusha makazi holela na migogoro ya ardhi hapo baadae.

Jerry Silaa

Katika kuhakikisha jambo hilo linakamilika kwa wakati Waziri Silaa ametoa wito kwa Makampuni binafsi yanayojihusisha na kazi za upangaji na upimaji kushiriki katika kazi hiyo ya kupanga na kupima maeneo yote yanayozunguka uwanja huo wa mpira wa miguu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!