Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) chapanua wigo wa kitaaluma nchini
Elimu

Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) chapanua wigo wa kitaaluma nchini

Spread the love

 

WAKATI maendeleo ya Elimu nchini yakiongezeka Chuo cha Uhasibu Arusha kimeongeza usanifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Mkuu wa Chuo hicho, Eleman Sedeka akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 18 ya vyuo vikuu yanayoendele katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam amesema kuwa AIA, imeongeza kozi nyingine nne ili kuhakikisha inaziba ombwe na mahitaji ya kitaaluma nchini.

“Sisi kama Chuo mwaka huu tunakuja na kozi nyengine mpya nne za ngazi ya shahada ambapo ni shahada katika usimamizi wa record maana ya (record and information managemant ) na shahada ya orditing intersurence,Accountance and finance na shahada mpya ya mass communication hii ni sahada mahususi kwaajili ya waandishi wahabari na wale watu wote wanao penda kujifunza mmbo mbali mbali kuhusu kuchakacha habari kuanzia kukamata habari,kuchakacha na kuzitoa”.

“Vile vile tuna kozi mpya ya Education management katika ngazi ya masters hii ni kozi imetengenezwa mahsusi kwaajili ya wale watu wanao fanya kazi katika sekta ya elimu sasa kwanini uje AIA kwa sasa hiv ndio chuo kinacho ongoza kwa kukua katika ubunifu katika jinsi tunavayo fanya mambo yetu”, aliongeza.

Chuo hicho cha Serikali kilichoanzishwa mwaka 1990 chenye Makao Makuu yake Arusha na matawi Babati, Dar es Salaam na Songea.

Chuo hicho kinachotamba na kozi za uhasibu kimekuja kuwika zaidi kilipoongeza kozi za Tehama, manunuzi , utalii .

Amesema kuwa kushiriki kwenye maonyesho hayo nu fursa kwa wazazi, walezi na Wanafunzi kujua zaidi kuhusu kozi zitolewazo na manufaa yake.

“Maonyesho haya ya TCU ni kwa ajili ya wanafunzi wazazi na walezi kuja kuongea na kujionea vyuo mbali mbali na kozi mbali mbali na kupata ushauri kutoka kwa wataalam kozi zipi wasome na kwa sababu gani kutokana na uwezo wao,malengo yao na matamanio yao”

Sedeka amesema kuwa Chuo hicho hakijaachwa nyuma na Teknolojia . Kimeanzisha programu maalum ya masomo kwa njia ya mtandao kwa wanafunzi wa Masters (online) ambapo mtu anaweza kusoma akiwa nyumbani.

mathalani wewe mwanafunzi wa shahada ya Uzamili unao uchaguzi wa kuingia darasani au unaweza kuingia ukiwa na laptop au vyote vikishindikana baadae usiku utakuta mafunzo yana kusubiri mtandaoni unaweza kutenga muse wake ukiwa nyumbani na utakuja chuo kufanya mtihani tu karibuni sana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!