CHAMA kikuu cha Upinzani nchini Sudani Kusini , kimejiondoa kwenye Baraza la ufuatiliaji wa amani nchini humo , kikishutumu vikosi vinavyohasimiana kwa mashambulizi yasiyo na msingi. Inaripoti BBC … (endelea).
Aidha chama hicho cha upinzani cha Sudani Kusini , People’ s Liberation Movement kilisema kuwa shambulio hilo la hivi punde la silaha , lilifanyika siku ya Jumatatu ya tarehe 21 machi 2022.
Hata hivyo, chama hicho kinaongozwa na Makamu wa Rais, Riek Machar ambaye miaka miwili iliyopita aliunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na aliyekuwa adui yake Salva Kiir.
Pia kuendelea kwa mvutano kati ya viongozi hao wawili , kumezuia kutekelezwa kwa makubaliano ya amani yenye lengo la kumaliza vita vya wenyewew kwa wenyewe, vya miaka mitano ambapo watu 400,000 wameuawa.
Leave a comment