September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TBA yaomba fedha kuendeleza maeneo yote ya kota

Mtendaji Mkuu wa TBA, Daudi Kondoro

Spread the love

 

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imeiomba Serikali kupitia Wizara ya ujenzi na uchukuzi kuendelea kutoa fedha za kuendeleza maeneo mengine yaliyorejeshwa Serikali Kuu kutoka Tamisemi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumatano tarehe 23 Machi 2022 na Mtendaji Mkuu wa TBA, Daudi Kondoro, wakati wa uzinduzi wa nyumba za Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.

Kondoro amesema watafanya hivyo kwa kuanzia na mikoa yenye uhitaji mkubwa wa makazi.
Alitaja maeneo hayo kwa mkoa wa Dar es Salaam ni Temeke kota, Ilala kota, Ukonga kota na Kinondoni Kota na Arusha kuna Kaloleni kota, Levolosi na Themi na Mwanza ni eneo la Ghana na Pemba.

Aidha amesema kuendeleza maeneo hayo itaiwezesha TBA kutekeleza kikamilifu ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi Ibara ya 55 inayoelekeza maeneo hayo kuendelezwa na TBA.

Pia amemthibitishia Rais Samia kuwa TBA imejipanga kutekeleza ujenzi wa majengo kwa ubora, gharama nafuu na kwamuda uliopangwa.

error: Content is protected !!