Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CCM Iringa yawataka wagombea wakubali kushindwa, wasiende kwa waganga
Habari za Siasa

CCM Iringa yawataka wagombea wakubali kushindwa, wasiende kwa waganga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Abel Nyamahanga akizungumza na wagombea 319 wa ubunge wa majimbo saba mkoani humo.
Spread the love

CHAMA cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kimetoa onyo kali kwa wagombea ubunge na udiwani watakaobainika kusaliti chama kwa kikiuka kanuni na taratibu za chama katika Uchaguzi Mkuu OKtoba 2020 watakatwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi tarehe 18 Julai 2020 na mwenyekiti wa CCM mkoani wa Iringa, Dk. Abel Nyamahanga wakati akizungumza na wagombea katika ngazi ya ubunge kwa majimbo saba na udiwani kata 106 Mkoa huo.

Nyamahanga amesema, mtia nia yeyote, kila mgombea anatakiwa kutambua katika uchaguzi kuna kupata na kukosa hivyo hawategemei baada ya kura za maoni kujitokeze maswala ya usaliti na makundi ya wagombea.

Amewataka wagombea kutambua masuala ya usaliti yamekuwa yakikigawa chama na kusababisha wapinzani kupata nguvu ya kuchukua majimbo jambo ambalo halikubaliki katika uchaguzi wa mwaka huu katika chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa.

Amesema nafasi ya ubunge waliyoomba ni ya utumishi hivyo ni vyema wakajitoa kwa moyo kuwatumikia wananchi na wana CCM kwa ujumla badala ya kufikiria kupata utajiri kupitia ubunge.

“Wagombea niwaeleze, hakuna mgombea ambaye yupo juu zaidi ya mwingine, wagombea wote wapo sawa hata wale wabunge wanaotetea nafasi zao, wote kwa sasa ni wanachama tu wa kawawida,’’ amesema Nyamahanga.

Amesema ndani ya CCM kuna miongozo ya kikanuni kwa watia nia pamoja na viongozi wa chama hicho ambayo ni mwiko kwa kiongozi yeyote kupendelea mgombea au mtia nia yeyote.

Soma zaidi..

Mwenyekiti huyo amesema, Chama Cha Mapinduzi kina nia njema na wagombea wote hivyo wanatakiwa kujenga imani na chama chao na hata ikitokea mmoja amepitishwa wengine wamuunge mkono ili kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo.

Amesema chama hakitamvumilia mgombea yoyote atakae mchafua mgombea mwingine kwakuwa, haijulikani jina lipi litarudishwa hivyo ikitokea mgombea aliyetukanwa akapitishwa chama kinapata wakati mgumu kumsafisha kipindi cha kampeni.

Baadhi ya wagombea wakisikiliza

Aidha wagombea wametakiwa kumtegemea Mungu zaidi badala ya kupishana kwa waganga wakienyeji ambao ndio wamekuwa chanzo cha migogoro katika chama baada ya kuwahakikishia ushindi baadae mambo yanakuwa tofauti.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Salim Abri Asas amesema, chama hakina mgombea maalum bali wagombea wote wapo sawa na watapita katika mchakato wa kikanuni ili kumpata mgombea mmoja atakaepigiwa kura na wajumbe.

Amesema anaamini katika mchakato huo wa kura za maoni, hakutakuwa na manung’uniko kwani kura zitapigwa za wazi na kila mgombea atahusika katika kuhesabu kura ili kuondoa malalamiko.

Katibu chama hicho Mkoa wa Iringa, Brown Mwangomale aliwataka wagombea kujiandaa kisaikolojia katika mchakato wa uchaguzi na kukubali kuwa katika uchaguzi kuna matokeo mawili ambayo ni kushinda na kushindwa.

Alisema kitendo cha kujiamini katika uchaguzi wa kura za maoni na badala yake matokeo ya kawa tofauti ndipo wanachama wanapogeukia katika usaliti jambo ambalo halikubaliki katika chama.

Alisema dhambi ya usaliti ni mbaya na adhabu yake kufukuzwa katika chama jambo ambalo halitarajiwi kujitokeza katika uchaguzi wa Oktoba 2020.

“Ndugu zangu, dhambi ya usaliti ni mbaya na kubwa, usaliti unaua na ndio maana vitabu vya dini vimekemea vikali usaliti,” alisema

Alisema CCM Mkoa wa Iringa wamedhamilia kushinda katika majimbo yote ya uchaguzi hivyo ushindi huo unatemewa zaidi na mshikamano utakaoneshwa na mshikamano wa wagombea wote 319 walioingia katika kuwania nafasi hiyo ya ubunge.

Mgawanyo wa majimbo ni; Iringa mjini wako 54, Isimani tisa, Kalenga 68, Kilolo 38, Mufindi Kasikazini 33, Mufindi Kusini 31 na Mafinga 20

Waliotia nia kugombea ubunge kupitia Mkoa, nafasi za vijana ni 13, wazazi nane, viti maalum wanawake 28, wafanyakazi wane, watu wenye ulemavu watano na wasomi watatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!