Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waliounga juhudi CCM njia panda
Habari za Siasa

Waliounga juhudi CCM njia panda

Spread the love

IWAPO Rais John Magufuli na Humphrey Polepole, watayaishi maneno yao kwamba ‘hakuna mbeleko’ kwenye mchakato wa uteuzi wa watia wa ubunge na udiwani ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ipo hatari ya wanasiasa waliounga juhudi kwenye chama hicho kuangukia pua. Anaandika Mwandishi Wetu, Dar es Slaam…(endelea).

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezo wa chama hicho, tayari wamejivua na kusisitiza ‘kila mmoja ajibebe.’

Msisitizo uliowekwa na viongozi hao wa juu ndani ya chama hicho, ni kwamba wagombea waliojipanga, kuishi na kuaminika na wanachama wa chama hicho, ndio wapewe ridhaa ya uwakilishi kwenye uchaguzi mkuu.

Taarifa zinaeleza, watia nia hao wageni ndani ya CCM, wamekuwa na wakati mgumu wa kushindana na wale waliotangulia na kujijenga kwa muda mrefu.

Mwaka 2016 hadi 2020, Tanzania imeshuhudia mvumo wa kipekee kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani kukimbilia CCM, wakidai kuunga juhudi za Rais Magufuli katika kulitumikia taifa.

Waunga juhudi hao, wengi wao wakiwa wabunge, madiwani na viongozi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF) na hata Chama cha ACT-Wazalendo, walihamia CCM na baadaye baadhi yao kusimamishwa kugombea ubunge katika maeneo waliyokuwa wakiyaongoza.

Jana tarehe 18 Julai 2020, Polepole akiwa mkoani Ruvuma katika mkutano wa utekelezaji wa Ilani ya chama hicho, amesema kila mgombea atajieleza na kupigiwa kura peupe na haki itasimama ili kuwa mfano Afrika.

“Kila mtu atajieleza, kujadiliwa na kupigiwa kura kwa haki. Tunataka utaratibu huu kuwa ni mfano Afrika,” amesema Polepole.

Kauli ya Polepole ilitanguliwa na ile aliyoitoa Rais Magufuli siku tatu zilizopita wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa na wilaya aliowaapisha katika Ikulu ya Jijini Dodoma.

“Nataka kuwathibitishia wananchi, wanaCCM, hakuna mtu yeyote aliyetumwa na mimi kugombea, hakuna mtu yeyote ametumwa na Makamu wa Rais, hakuna mtu yeyote ametumwa na Waziri Mkuu, hakuna mtu yeyote aliyetumwa na Mzee Mangula (Philip Manguka), hakuna mtu yeyote aliyetumwa na Katibu Mkuu Dk. Bashiri (Dk. Bashiru Ally).

“Kwa hiyo, kama wapo watu wanasema mimi nimewatuma, ni waongo. Na hii meseji iwafikie wanaCCM wote. Nyinyi wapimeni wagombea kulingana na nyinyi mnavyoona,” amesema Rais Magufuli.

Kitila Mkumbo, mtia nia jimbo la Ubungo (CCM)

Waunga juhudi hao CCM, wamechukua fomu za kugombea ubunge na hata udiwani kupitia chama hicho. Baadhi yao wakibaki kwenye majimbo yao ya awali na miongoni mwao wamehama jimbo.

Miongoni mwa waunga juhudi waliochukua fomu kugombea ni Peter Lijualikali (Kilombero), David Silinde, aliyekuwa Jimbo la Momba sasa anagombea Jimbo la Tunduma, wote walikuwa Chadema.

Wengine ni Kalist Lazaro aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha (Chadema), amechukua fomu CCM kugombea Jimbo la Arusha Mjini. Samson Mwigamba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo alitimikia CCM na sasa analitaka jimbo la Arsuha Mjini.

Prof. Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, anagombea ubunge Arusha Mjini, huna anakutana na aliyukuwa mwanasheria wa chama hicho Wakili Albert Msando.

Wamo pia Abdallah Mtolea aliyekuwa CUF katika Jimbo la Temeke, alikimbilia CCM Novemba 2020 na sasa anagombea jimbo hilo. Maulid Mtulia aliyepata ubunge wa Kinondoni kupitia CUF, tarehe 2 Desemba 2017 alikimbilia CCM na sasa amechukua fomu ya nia ubunge kupitia chama hicho.

Joshua Nassari aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia Chadema, amerudi kwenye jimbo hilo kupitia CCM. Dk. Vincent Mashinji aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema, amejitoksa kwenye Jimbo la Kawe kupitia CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!