October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rafu CCM zatikisa Shinyanga

Donald Magesa ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga

Spread the love

WATIA nia ya ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameanza kuchezeana rafu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga…(endelea).

Kutokana na rafu hizo, Donald Magesa ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ametishia kufuta mchakato wote kuanzia kuchukua fomu hadi kurejesha.

Akiwa kwenye kikao cha dharura na watia nia hao, amesema baadhi yao wameanza kuwafuata wapiga kura za maoni majumbani mwao, na kuwashawishi kwa namna wanavyoweza ili wawapigie kura na hatimaye kuteuliwa.

Akizungumzia tukio hilo, Magesa amesema, jimbo hilo lina wapiga kura 449 na kuwa, vijana wengi ndio waliojitokeza huku robo tatu yao wakiwa na elimu ngazi ya Shahada.

“Baadhi yenu mmenichefua, kwani mnawazungukia wajumbe na kutaka kushiriki kwenye vitendo vya rushwa. CCM inataka viongozi halisi na sio watoa fedha,” amesema Magesa na kuongeza “kutoa fedha sio kigezo cha kuchaguliwa hasa kama mtu hafuati kanuni.”

Amesema, mkoa huo wote wenye majimbo matano, waliochukua fomu Ushetu (18), Kahama Mji (70), Shinyanga Mjini (60), Msalala (44) na Solwa (54), na kwamba kati ya waliochukua fomu 324, wanaume ni 298 na wanawake ni 26.

error: Content is protected !!