Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG abaini madudu katika vyama 10 vya upinzani
Habari za Siasa

CAG abaini madudu katika vyama 10 vya upinzani

Spread the love

UKAGUZI wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichele, kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, umebaini madudu katika vyama 10 vya siasa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ripoti ya ukaguzi huo iliyowasilishwa leo Jumatatu, bungeni jijini Dodoma, inaonesha Chama cha Kijamii (CCK), Natinal League For Democracy (NLD), NCCR-Mageuzi, African Democratic  Alliance (ADA TADEA) na Union for Multiparty Democracy (UMD), vilikiuka sheria ya vyama vya siasa kwa kutowasilisha benki Sh. 104.08 milioni, fedha zilizokusanywa kutoka kwa wanachama wake.

“Vyama hivyo vilikusanya michango kutoka kwa wanachama mbalimbali jumla ya Sh. milioni 104.08 bila kuziwasilisha katika akaunti za benki za vyama husika. Hii ni kinyume na kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Vyama vya Siasa [Sura ya 258 iliyorekebishwa mwaka 2019] kinachotaka kila chama cha siasa, ambacho kimesajiliwa kisheria kufungua akaunti ya benki ya chama, ambayo mapato yote yanayopatikana kuwasilishwa benki,” imesema ripoti hiyo.

Wakati vyama hivyo vitano vikishindwa kuwasilisha benki fedha hizo, ukaguzi wa CAG umebaini vyama vinne, Alliance for Africa Farmers Party (AAFP), Demokrasia Makini (DM), National Reconstruction Alliance (NRA) na National League for Democracy (NLD), havikuwasilisha tamko la kila mwaka la mali inavyozimiliki kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini .

Katika hatua nyingine, ripoti hiyo imesema Chama cha Wananchi (CUF),kilipata hati yenye shaka, wakati NRA ikipata hati mbaya, huku CAG akishindwa kutoa maoni kwa AAFP.

“Taarifa za fedha za CUF hazikujumuisha baadhi mali za chama. Taarifa ilionesha tu kuwa chama kinamiliki mali lakini thamani ya mali hizo haikujumuishwa katika taarifa za fedha. Jambo hili ni kinyume na matakwa ya aya ya 26 na 27 ya IPSAS 17 (Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu katika Taasisi za Umma) na kanuni ya 22(1) ya Kanuni za Uandaaji wa Taarifa za Fedha za Vyama vya Siasa za Mwaka 2019. Hivyo, thamani ya mali zilizooneshwa katika taarifa za fedha za CUF hazikuonesha uhalisia wa mali zake zote,” imesema taarifa ya CAG.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!