Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Makusanyo ya Serikali mwaka 2022/2023 yapaa kwa 9%
Habari Mchanganyiko

Makusanyo ya Serikali mwaka 2022/2023 yapaa kwa 9%

Spread the love

MAKUSANYO ya Serikali katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 yameongezeka kwa Sh. 3.582 trilioni, hadi kufikia Sh. 41.880 trilioni, kutoka Sh. 38.398 trilioni yaliyokusanywa 2021/2022. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ongezeko hilo limebanishwa katika ripoti kuu ya ukaguzi wa Serikali kuu kwa 2022/2023, uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, ambayo imewasilishwa leo tarehe 15 Aprili 2024, bungeni jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, makusanyo yanayotokana na kodi, yasiyotokana na kodi na makusanyo ya halmashauri yaliyofadhili bajeti kwa Sh. 26.515 trilioni (63%), wakati yanayotokana na misaada na mikopo ni Sh. 15.365 trilioni (37%).

“Katika mwaka wa fedha wa 2022/23, Serikali ilikusanya Sh. trilioni 41.880, zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa ya Sh. trilioni 41.480, ikiwa ni ongezeko la makusanyo kwa Sh. bilioni 400. Aidha, nilibaini ongezeko la makusanyo la Sh. trilioni 3.582, sawa na asilimia tisa ikilinganishwa na Sh. trilioni 38.298 zilizokusanywa katika mwaka wa fedha uliopita wa 2021/22,” imesema ripoti hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!