Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge la Chadema lapata viongozi wapya
Habari za Siasa

Bunge la Chadema lapata viongozi wapya

Susan Lyimo
Spread the love

SUSAN Lyimo amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Wananchi wa Chama cha Chadema, huku Lumola Kahumbi, akichaguliwa kuwa Naibu Spika wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Viongozi hao wamechaguliwa katika uchaguzi wa Bunge hilo, uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana tarehe 15 Desemba 2022.

Susan alishinda katika uchaguzi wa nafasi ya Spika kwa kupata kura 50, dhidi ya mpinzani wke aliyekuwa natetetea kiti hicho, Celestine Simba, aliyepata kura 35.

Naye Kahumbi alishinda kwa kupata kura 69, dhidi ya mpinzani wake Shija Shibeshi, aliyepata kura 16. Watu waliopiga kura walikuwa 85.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, aliushukuru uongozi uliopita kwa kazi nzuri waliofanya huku akiutaka uongozi mpya kutekeleza majukumu yake katika kukijenga chama hicho.

“Chama kina wajibu mkubwa tunachohitaji tujipange kila mmoja atekeleze wajibu wake katika kuijenga taasisi yetu pendwa ya Chadema. Hatupaswi kuendelea kulia kwa mabaya ambayo tumeshayapitia, tunapaswa kujiimarisha kuitengeneza kesho yetu iliyobora zaidi,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Siri ya mafanikio ya chama hiki sio kupigania fedha ndani ya chama ila ni ule mshikamano wetu ndiyo nguvu ya kuitetea ajenda zetu. Naomba muendeleze mshikamano lakini tusishikamane bila wajibu.”

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Spika aliyemaliza muda wake, Celestine aliupongeza uongozi mpya huku akihidi kuupa ushirikiano.

“Nafurahi kwamba nimechora ramani sasa wajenzi waendelee, tutaunga mkono na kama mtu haelewi tutamwambia hapa umekosea hapana. Niko tayari kushirikiana na viongozi waliopo kuhakikisha Bunge la Wananchi linaendelea kuwa sauti ya wananchi kwelikweli,” alisema Celestine.

Spika mpya, Susan ameahidi kulifanya bunge hilo kuwa imara katika kuwasemea wananchi pamoja na kuishauri Serikali juu ya namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.

“Cha kwanza naenda kuanza nacho kuhakikisha kwamba tunakuwa na Bunge moja imara litakalokuwa na sauti ya wananchi na itakutana na kamati ya uongozi tuone namna gani tunakuwa na muundo ambao tutafanya wabunge wote washiriki kikamilifu sababu tunajua hatuna uwakilishi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huu ndio uwakilishi wetu kusimamia na kushauri Serikali,” alisema Susan.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!