Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kiongozi wa waasi agonga mwamba ICC
Kimataifa

Kiongozi wa waasi agonga mwamba ICC

Spread the love

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), iliyopo mjini The Hague, nchini Uholanzi, imetupilia mbali rufaa ya kiongozi wa zamani wa waasi kutoka kundi la Lord’s Resistance Army (LRA), Dominic Ongwen. Anaripoti Saed Kubenea…(endelea).

Ongwen alikuwa amewasilisha rufaa mahakamani hapo kupinga hukumu ya miaka 25 gerezani dhidi yake.

Dominic Ongwen, anayefahamika kama White Ant, alipatikana na hatia kwenye makosa zaidi ya 60, ikiwamo uhalifu dhidi ya binadamu, ubakaji, utesanyaji wa kongono na uhalifu wa kivita.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama, Ongwen sasa atalazimika kutekeleza adhabu hiyo.

Maelfu ya watu nchini Uganda, wanaripotiwa kuuawa na wafuasi wa kundi hilo.

Waendesha mashitaka wa ICC walisema, Ongwen amepewa adhabu ndogo kulingana na makosa aliyotenda, kutokana na ukweli kuwa naye alikuwa mhanga baada ya kutekwa na LRA akiwa mtoto mdogo.

Kundi hilo la waasi liliundwa zaidi ya miaka 30 iliyopita, likiendesha shughuli zake nchini Uganda na mataifa jirani.

Majaji waliosikiliza rufaa hiyo, wamepinga hoja za Ongwen juu ya maisha yake ya hapo awali wakati alipokuwa mtoto na madai yake kwamba alikuwa mgonjwa wa akili.

Wamesema Ongwen alikuwa na dhima maalumu katika kutenda ukatili.

Ongwen, aliyezaliwa mwaka 1975 katika kijiji cha Choorum wilaya ya Amuru kaskazini mwa Uganda, alitekwa nyara na kundi la waasi wa Josephy Kony – LRA  – alipokuwa  mtoto wa miaka tisa.

Kulingana na maelezo ya mama yake, Ongwen alitekwa nyara akiwa na umri wa miaka 9 hadi 10, wakati akielekea shule ya msingi Abili Koro, mwaka 1988.

Alibebwa hadi kwenye kambi ya LRA, kutokana na kushindwa kutembea umbari mrefu.

Mama yake Ogwen alipofahamishwa habari za kutekwa nyara kwa mtoto wake, aliamua kuwafata wafuasi hao, na badaaye watu walimkuta mama huyo amefariki pamoja na mumewe.

Baada ya muda akiwa na umri wa miaka 18, Ogwen alipewa cheo cha Brigadier wa kundi la LRA na kuongoza kikosi cha Sinia.

Anadaiwa kushirika katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa kivita, na kwamba Mei 2004, walishambulia kambi ya ndani ya Lukodi wilayani Gulu, kaskazini mwa Uganda.

Pia alishambulia kambi nyingine za ndani ikiwemo ya Pajule, Odeke na Abok na kushiriki mauaji mbalimbali ya wanchi wasiokuwa na hatia, ubakaji na unyanyasaji wa kigono.

Watu zaidi ya 400,000 wanaripotiwa kuuliwa na watoto wapatao 60,000 walitekwa nyara na magaidi wa LRA.

Kiongozi wa zamani wa waasi na kamanda anayeogopewa wa jeshi la LRA, ni mfuasi wa kwanza wa kundi hilo, kufikishwa katika mahakama hiyo.

Alikabiliwa na makosa 70 ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, lakini aliondolewa baadhi ya mashtaka.

Kesi hii ilisababisha mahakama kuwa katika njia panda kwani alionekana kuwa mwathiriwa na pia mhalifu.

Alisema kuwa alitekwa na LRA na kulazimishwa kuwa mwanajeshi akiwa mtoto, kabla ya kupanda akishika nafasi mbalimbali mpaka kuwa Naibu kamanda wa Kony.

Lakini akisoma uamuzi wake, jaji anayesimamia kesi hiyo, Bertram Schmitt alisema: “Hatia yake imethibitishwa bila shaka yoyote.”

Alihukumiwa kwa makosa kadhaa ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, mateso, utumwa wa kingono na uporaji.

ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwake mwaka 2005 na Marekani na vikosi vya Afrika wamekuwa wakimtafuta tangu mwaka 2011.

Mwaka 2014 alijisalimisha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na kesi yake iliyodumu kwa miaka mitatu na nusu huko The Hague ilipomalizika Machi mwaka huu.

Mawakili wake walikuwa wameomba aachiliwe na walinukuliwa na shirika la habari la Reuters wakisema, katika hoja ya kuhitimisha, kwamba “wakati Ongwen alitekwa nyara hakuwa na cha kufanya, alifanywa mtumwa. Utumwa huo uliendelea hadi alipoondoka msituni.”

Lakini waendesha mashitaka walisisitiza kuwa alikuwa mtu mzima wakati wa makosa hayo hivyo haiwezekani kutowajibishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!