Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Biteko azindua zahanati Ilala, 12,000 kufaidika
Afya

Biteko azindua zahanati Ilala, 12,000 kufaidika

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dk. Doto Biteko amezindua Zahanati ya Bungoni iliyopo mtaa wa Mafuriko Ilala  jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi kutumia fursa ya  uwepo wa huduma ya zahanati hiyo.

Amewataka wananchi kutokwenda mbali kufuata huduma za afya, kwani ni dhamira ya Serikali kusogeza huduma kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza katima hafla ya uzinduzi huo leo tarehe 29 Disemba 2023, Dk. Bitenk aliwataka wananchi wa Ilala kumpa ushirikiano mbunge wao kwa vitendo na kumpongeza kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuleta maendeleo.

Pia amewataka viongozi wengine kuiga mfano wa mbunge huyo kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo na kukemea wachache wanaojificha kwenye kivuli cha taratibu kuchelewesha maendeleo.

Ujenzi wa zahanati hiyo ulianza Februari mwaka huu, kwa jitihada za wananchi na baadae Serikali na umegharimu kiasi cha Sh milioni 351.

Ujenzi huo umehusisha gharama za ujenzi, samani, dawa na vifaa tiba na umefadhiliwa na African Relief Agency na Taasisi ya Rahma International kutoka Kuwait na inamilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali.

Aidha, Dk. Biteko alipata fursa ya kutembelea jengo hilo linalohusisha wagonjwa wa nje yani OPD, Kliniki ya Baba, Mama na Mtoto pamoja na jengo la kujifungulia na kusalimiana na kinamama waliojifungua kwenye Zahanati hiyo.

Zahanati hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia kata nne zilizopo wilaya ya Ilala ambazo ni Ilala, Buguruni, Sharifu Shamba, na Mchikichini wapatao Elfu 12.

Akizungungumza wakati wa hafla hiyo, Mbunge wa Ilala na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azan Zungu (CCM) amewataka watendaji kuhakikisha wanatumia vyema fursa za wafadhili wanaokuja kuwekeza Kwenye sekta ya Afya na kuondoa mikwamo inayoweza kuchelewesha maendeleo.

Amesema, wilaya ya Ilala inapokea wageni wengi kwa siku, sambamba na wananchi wenye mahitaji kwenye Sekta ya Afya hivyo uwepo wa vituo hivi utasaidia kuboresha utoaji wa huduma.

Awali, akitoa taarifa ya mafanikio ya Idara ya Afya kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji Dk. Zaituni Hamza amesema kuwa, wamefanikiwa kujenga jumla ya vituo vipya saba vya kutolea huduma na kupandisha hadhi zahanati tano kuwa vituo vya Afya, hivyo kufanya jumla ya vituo vya Afya kuwa 12.

Aliongeza kuwa kuelekea mwaka wa mama 2025,  imekuja na miradi ya kimkakati ikiwemo uanzishwaji wa Chuo cha Afya cha Kati na Sayansi Shirikishi hospitali ya wilaya ya Kivule ambapo jengo la kwanza tayari limeshapauliwa, lengo ni kuunga mkono azma na dhamira ya Mheshimiwa Rais kuwaletea maendeleo karibu wananchi wake.


Aidha, Dk. Zaituni alimshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kuongeza bajeti kwa Wizara ya Afya  hususan upatikanaji wa dawa na vigaa tiba kutoka asilimia 90.1 hadi kufikia asilimia 94 na kumuahidi Mheshimiwa Rais kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

error: Content is protected !!