Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yamuita Mdee na wenzake
Habari za SiasaTangulizi

ACT-Wazalendo yamuita Mdee na wenzake

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimefungua milango kwa wabunge viti maalum 19 waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wajiunge nacho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 29 Disemba 2023 na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo,Ado  akizungumza na Mwanahalisi Online ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa, chama chao kipo tayari kuwapokea hususan kiongozi wao Halima Mdee, kwa kuwa ni majembe.

“Tukimuona mtu ni jembe mathalani kina Halima Mdee wana mgogoro na chama chao wakiamua kwamba wanataka kujiunga na ACT-Wazalendo, tutawapokea na kuwapa nafasi sababu tunaamini wanasifa,” amesema Ado.

Ado amesema “katika siasa wanasiasa wanaweza kujikwaa kwa hili na lile, chama kinabidi kipime na nikitazama wanawake hawa 19 ni ishara ya ukomavu.”

Ado ametoa wito huo wakati akizungumzia athari za kupokea wanasiasa kutoka vyama vingine, ambapo amesema kitendo hicho kiliwaathiri baada ya kumpokea aliyekuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Hayati Benard Membe, kisha kumteua kuwa mgombea wake urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, ambapo baadae alirejea alikotoka.

“Tumejifunza juu ya hilo, kitendo cha Membe kurejea CCM kinapaswa kutufundisha vyama vya upinzani kwamba ni lazima kwa nafasi nyeti ya urais tuandae makada wetu watakaokuwa tayari kuvumilia changamoto za upinzani badala ya kila baada ya uchaguzi wanarejea CCM,” amesema Ado.

Hata hivyo, Ado amesema ACT-Wazalendo iko tayari kupokea wanachama kutoka vyama vingine kisha kuteua kuwa wagombea baada ya kuwafanyia tathimini ya kina kuona kama wanafaa, lakini hakiko tayari kupokea mwanachama wa chama kingine kisha kuwateua kuwa wagombea urais wa chama hicho.

Hatua ya ACT-Wazalendo kuwafungulia milango wabunge hao viti maalum waliofukuzwa Chadema Novemba 2020, imekuja wiki mbili baada ya Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, kutoa hukumu dhidi ya kesi waliyofungua kupinga kuvuliwa uanachama.

Mahakama hiyo iliamuru Chadema kuitisha tena kikao cha Baraza Kuu lake kwa ajili ya kusikiliza tena rufaa zao za kupinga kufukuzwa ili haki itendeke.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!