March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Biashara za Saudia, Emirates, Bahrain, Misri zazuiwa Qatar

Spread the love

MGOGORO wa Qatar na mataifa jirani unazidi kukua na sasa taifa hilo (Qatar) limezuia kuingizwa biashara kutoka Saudi Arabia, Emirates, Bahrain na Misri. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Sheikh Ahmed Jassem bin Mohammed Al Thani ambaye ni Waziri wa Uchumi na Biashara wa Qatar ameagiza sekta zote nchini humo kuacha kuagiza na kununua bidhaa yoyote inayotoka miongoni mwa nchi hizo.

Waziri huyo amesema kuwa, serikali itaendesha msako ili kujiridhisha kama agizo hilo limetekelezwa sana na namna lilivyokusudiwa na kwamba, atakayebainika kukiuka, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Serikali ya Qatar imeeleza kushinda vikwazo vya awali vilivyowekwa Bahrain, Saudia, Emirates na Misri.

Juni mwaka jana Bahrain, Saudi, Bahrain, Emirates na Misriziliitenga Qatar kwa madai kusaidia ugaidi jambo lililoenda sambamba na kufunga mipaka yao.

error: Content is protected !!