Saturday , 20 April 2024
Habari MchanganyikoTangulizi

Tanesco lawamani

Makao Mkuu wa Tanesco, Ubungo Dar es Salaam kabla hayajavunjwa
Spread the love

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) linatuhumiwa kuwalipisha wananchi malipo ya kuingiziwa umeme majunbani mwao bila kuwapa huduma husika kama ilivyo ahidi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Wananchi wa kitongoji cha Namanga kata ya Mvuti manispaa ya Ilala, ndio wenye malalamiko hayo.

Baadhi ya wananchi waliokumbwa na mkasa huo, wamemweleza mwandishi kuwa, wamefanya malipo kwa ajili ya kuvutiwa umeme tangu Frebuari mwaka huu, na waliahidiwa kuingiziwa umeme wiki mbili baada ya kufanya malipo lakini mpaka sasa hawajapata walichoahidiwa.

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Namanga, Masunga Halawa amesema wananchi walilipa gharama za Tanesco kama walivyotakiawa kufanya kwa ahadi ya kuwekewa umeme, lakini mpaka sasa hawajui kilichowakwamisha Tanesco kutimiza wajibu wao.

“Watu wamejibana ili kupata pesa za kulipia gharama za umeme, wakafuata utaratibu walioelekezwa na Tanesco, baada ya kuwalipa wametuacha ‘solemba’ bila kujua hatma yetu.” Amesema Halawa na kuongeza…

“Kuna watu wamekubali kuharibu mazao yao ili jamii yetu ipate umeme, lakini leo tukiwauliza Tanesco kila mmoja anajibu anavyojisikia.:

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Sikuzani Madenge, amesema Tanesco imekuwa ikiwazungushwa bila kuwapa sababu za kufanya hivyo, ingawa wameshalipia kama walivyotakiwa kufanya.

“Mimi na baadhi ya wenzangu tumeingia gharama kubwa ili kuhakikisha tunapata huduma ya umeme, lakini kinachoendelea sicho tulichoahidiwa,” anasema Salumu Mdigwa, mwenye umri wa miaka 50.

Salum amesema, ile ndoto yao ya kuona zaidi ya Kaya 500 zilizopo kwenye mtaa huo zinapata umeme zimeanza kuyeyushwa na Tanesco.

“Hatujui Tanesco wana shida gani, ni afadhali wangekuja kutuambia kinachowakwamisha kuliko kukaa kimya,” anasema Rasuli Bandio, mkazi mwingine wa mtaa wa Namanga.

Afisa Mahusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amesema atawasiliana na ofisi za Tanesco zinazohudumia eneo hilo ili kujua tatizo.

Leila alikuwa akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua sababu za wananchi kuilalamikia Tanesco.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!