Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Biashara ‘BetPawa Dream Maker’ kutimiza ndoto miradi 20 ya kijamii
BiasharaHabari Mchanganyiko

‘BetPawa Dream Maker’ kutimiza ndoto miradi 20 ya kijamii

Spread the love

Jumla ya miradi 20 inayohusu masuala ya afya, usafi wa mazingira, maji, ujasiriamali na ubunifu imechaguliwa katika awamu ya pili ya kampeni ya Dream Maker iliyokuwa wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi kushiriki. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kampeni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya ubashiri BetPawa Tanzania, ilifanyika kuanzia Oktoba mwaka huu kupitia basi maalum lililojulikana kama Dream Bus ambapo wakazi wa Lindi, Mtwara na Ruvuma walipewa fursa ya kupanda kwenye basi na kuelezea ndoto au mawazo yao ya miradi.

Maombi mengine yalitumwa kwa njia ya mtandao kupitia video, kurasa za mitanado ya kijamii kwa kutumia hastag #betPawaDreamMaker.

Akiwatambulisha washindi 20 wa msimu huu wa pili wa BetPawa DreamMaker jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Borah amesema kuwa miradi hiyo 20 bunifu ilitokana na mamia ya ndoto na mawazo mbalimbali ya miradi kutoka kwa  washiriki tofauti iliyokusanywa kupitia kampeni hiyo.

“BetPawa ilipitia kila ndoto kabla ya kuchagua ndoto 20 bora za kusaidia na kuzifanya kuwa kweli” aliongeza.

Alisema DreamMaker inamwezesha  Anania Muba kutoa huduma bora na salama zaidi za afya katika zahanati ya  Nangomba mkoani Mtwara.

Anania ana ndoto ya kukamilisha ujenzi wa jengo la zahanati hiyo na kwamba jengo linalotumika sasa limeharibika na si salama kwa ajili ya kutoa huduma za afya.

“Nawashukuru BetPawa kwa kukubali kutimiza ndoto yangu ya kuchangia ujenzi huu utakaoboresha maisha ya mamia ya wakaazi wa eneo hili wanaotegemea kliniki hii kwa ajili ya huduma zao za afya,” amesema.

Herman Mwakatobe mkazi wa Mbeya sasa anajiandaa kufungua kiwanda kinachotengeneza majiko rafiki kwa mazingira yanayotumia mafuta yaliyotumika ya vilainishi/ oili chafu kama nishati mbadala ya kupikia.

Anatarajia kuwa majiko hayo yatatumika  nyumbani, migahawani, shuleni, vyuoni, na katika viwanda vya sabuni, ili kulinda mazingira kwa kupunguza ukataji miti na kutumia nishati hiyo mbadala

“Nikifanikiwa kutimiza ndoto yangu, nitatoa ajira kwa jamii katika kiwanda changu na sokoni, na nitaita jiko hilo Pawa,” Mwakatobe amesema.

BetPawa pia itamwezesha Eric Salema kushughulikia tatizo la uhaba wa maji Sanya Juu, Kilimanjaro kwa kujenga kisima na kuvuta maji kutoka kwenye kisima hicho ili kusaidia wakulima na wafugaji wa jumuiya hiyo.

“Nafurahi kuwa BetPawa watatuwezesha kupata maji ya uhakika ambayo yatatusaidia kulima mboga na kunywesha mifugo yetu, ili kuboresha maisha yetu wote,” amebainisha.

Washiriki wengine ambao ndoto zao zitatimia ni pamoja na Khadija Bundala wa Dar es Salaam atakayepata bajaji mpya kwa ajili ya biashara.

Makusanyo ya biashara yatamsaidia kumpeleka mwanae kupata huduma za afya za kila mwezi katika kliniki ya wagonjwa wa seli mundu (sickle cell), kulipia dawa anazotumia kila siku, pamoja na huduma za uhakika za chakula na ada ya shule.

Vile vile, BetPawa DreamMaker itatimiza ndoto ya Delphinus Magezi ya kufungua karakana ya uhunzi, uchomeaji vyuma na kutengeneza vifaa vya aluminium pamoja na kutoa mafunzo kwa vijana 20 kila mwaka, ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana jijini Dodoma.

“Naye Samson Lazaro wa Kahama anayeota kuwa na studio ya kurekodi muziki, pamoja na Eric Kimena wa Dar es Salaam mwenye maono ya kumiliki studio ya video na picha wote sasa wapo karibu kupaa na kutimiza malengo yao kwa nguvu za BetPawa DreamMaker,” Borah alimalizia.

Meneja masoko wa BetPawa Tanzania, Borah Ndanyungu amesema Dream Maker ya betPawa inaendelea kubainisha na kutimiza ndoto za Kitanzania zenye ushawishi kuwa kweli.

Msimu uliopita wa kwanza wa BetPawa Dream Maker ulifanyika September 2021 na kubainisha ndoto za nyumba, biashara na huduma za michezo zinazoendelea kunufaisha maisha ya jamii na kuibua fursa mpya za biashara kote nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Pata Mil 450 ya Non Stop Drop ukicheza Meridianbet kasino

Spread the love  JIUNGE na promosheni ya Kusisimua iitwayo NON-STOP DROP, inayotolewa...

Biashara

Exim Bank yaendeleza malipo ya kidijitali na Chef’s Pride Dodoma

Spread the love  BENKI ya Exim imeingia makubaliano na Mgahawa wa Chef’s...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!