Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Benki ya Dunia yaonesha wasiwasi juu mikopo ya China kwa Afrika
Kimataifa

Benki ya Dunia yaonesha wasiwasi juu mikopo ya China kwa Afrika

Spread the love

 

RAIS wa Benki ya Dunia (WB), David Malpass amesema ana wasiwasi kuhusu baadhi ya mikopo ambayo China imekuwa ikitoa kwa nchi zinazoendelea kiuchumi barani Afrika. Vinaripoti vyombo vya Habari vya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa BBC, Malpass alinukuliwa akisema kuwa kinachomtia wasiwasi ni hali ya usiri wa masharti na sheria za mikopo hiyo na kuhitaji ziwe wazi.

Wasiwasi wa Malpass umekuja baada ya nchi ya Ghana na Zambia kutakiwa kulipa madeni yao kwa serikali ya China ikiwa yenyewe inadai kuwa mikopo hiyo inatolewa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Nchi zinazoendelea mara nyingi hukopa pesa kutoka kwa mataifa mengine au mashirika ya kimataifa ili kufadhili sekta ambazo zitakuza uchumi wao kama vile miundombinu, elimu na kilimo.

Kwa mujibu wa BBC, ongezeko kubwa la viwango vya riba nchini Marekani na mataifa mengine makubwa kiuchumi kwa mwaka jana kunafanya ulipaji wa mikopo kuwa ghali zaidi kwa sababu ukopaji mwingi unafanywa kwa fedha za kigeni kama vile dola za Marekani au euro.

Wachambuzi wanaeleza kuwa pamoja na mikopo hiyo kuwa ya kisheria lakini nchi zinazoendelea kiuchumi zinashindwa kumudu mikopo hiyo.

Malpass ameeleza kuwa kitendo hicho kitaufanya uchumi wa nchi hizo kushindwa kukua kwa kasi.

Kukabiliana na changamoto hiyo na matokeo ya ziara ya wiki hii ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris katika nchi tatu za Afrika. Ni ziara inayokuja na ahadi kubwa za msaada wa kifedha kwa Tanzania na Ghana.

Wachambuzi wanaeleza kuwa China inaongeza ushawishi kwenye bara hilo kwa kutazama fursa hasa kwenye malengo yake ya kutengeneza gari za umeme. China inalitazama Bara la Afrika kama bara lenye maliasili, madini ambayo ni pamoja Nikeli, inayotengeneza betri zinazotumika kwenye gari za umeme.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!