Saturday , 11 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bei ya vyakula yashuka, kodi ya pango na ‘guest’ yaongezeka
Habari Mchanganyiko

Bei ya vyakula yashuka, kodi ya pango na ‘guest’ yaongezeka

Spread the love

 

BEI ya bidhaa za vyakula kwa mwezi Agosti 2021, ilipungua huku ya bidhaa zisizo za vyakula ikiwemo mavazi, kodi ya pango na nyumba za kulala wageni ‘Guest House’, zilipanda. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo ilitolewa jana Jumanne, tarehe 8 Agosti 2021 na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruthi Minja, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

Minja alisema, mfumo wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti 2021, umepungua hadi kufikia asilimia 3.6 kutoka asilimia 5.1, iliyokuwa Julai 2021.

“Kwa mfano baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei ni pamoja na nafaka, bidhaa za nafaka zilizopungua ni kama mahindi na unga wa mahindi kwa asilimia 7.2, nyama ( 6.3%) ,mbogamboga (2.3%) na maharagwe (4.7),” alisema Minja.

Alisema, mfumuko wa bei usiojumuisha bidhaa za vyakula na vinywaji baridi katika kipindi hicho, uliongezeka kutoka asilimia 3.3 Julai 2021 hadi kufikia 4.0 Agosti mwaka huu.

“Mfumuko wa bei ambao haujumuhishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi, kwa Agosti 2021 umeongezeka hadi asilimia 4.0, kutoka asimia 3.3 ilivyokuwa kwa mwaka unaoishia Julai 2021,” alisema Minja.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruthi Minja

Pia, alisema bei ya mavazi imeongezeka kwa asilimia 4.7, wakati bei ya kodi ya pango ikipanda kwa asilimia 5.1 na nyumba za kulala wageni imepanda kwa asilimia 5.3.

“Kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizokuwa za vyakula zilizoongezeka bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 4.7, mkaa kwa asilimia 1.9, gesi asilimia 2.1, Kodi ya Pango kwa asilimia 5.1 na gharama za malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.3,” alisema Minja.

Hata hivyo, Minja alisema mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Agosti 2021, umebaki kuwa wa asilimia 3.8 kama ilivyokuwa Julai 2021.

Minja alisema hatua hiyo ina maanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2021, imekuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai 2021.

“Mfumko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2021 umechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa mfumko wa bei wa baadhi ya bidhaa ya vyakula na bidhaa zisizo za vyakula,” alisema Minja.

Akizungumzia mfumko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia Agosti 2021, Minja alisema nchi ya Kenya mfumuko wa bei katika kipindi hicho umeongezeka hadi asilimia 6.57, kutoka asilimia 6.55, kwa mwaka ulioishia Julai 2021.

Aidha, alisema nchini Uganda mfumuko wa bei katika kipindi hicho umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1, kwa mwaka ulioishia Julai 2021.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi NBS, Daniel Msolwa, alisema mwenendo wa viashiria vya uchumi vya muda mfupi kuanzia Januari hadi Juni 2021, umeendelea kuimarika licha ya uwepo wa changamoto za Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19).

Msolwa alisema idadi ya Watalii Imeendelea kuongezeka, ambapo kati ya Januari hadi Juni kiwango cha watalii walioingia nchini kiliongezeka kuwa asilimia 4.5, ikilinganishwa na kiwango hasi cha asilimia 43.6 kipindi kama hicho mwaka 2020.

“Idadi ya watalii walioingia nchini mwezi Juni 2021 walikuwa 57,689 ikilinganishwa na 9,671 walioingia nchini mwezi Juni 2020,” alisema Msolwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waitara ahoji bungeni mwarobaini mauaji katika mgodi Barick North Mara

Spread the loveMBUNGE wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara, ameitaka Serikali kutafuta...

error: Content is protected !!