Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Biashara United kupaa leo, kuwavaa wadjibout
Michezo

Biashara United kupaa leo, kuwavaa wadjibout

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Biashara United ya mkoani Mara inatarajia kuondoka leo 9 septemba 2021majira ya saa 10:00 jioni chini kuelekea nchini Djibout kwa ajiri ya mchezo wake wa kwanza wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu ya Dhikhil Fc. Anaripoti Damas Ndelema TUDARCo(endelea)

Mchezo huo wa hatua ya awali utapigwa kesho, majira ya saa 10 jioni, kwenye Uwanja wa Stade du ville.

Hapo awali Biashara United ilitakiwa kuondoka nchini siku ya jana kwenda nchini Djibout lakini ilishindikana kutokana na baadhi ya wachezaji kuchelewa kutoka kwa hati zao za kusafiria  jambo lililofanya safari hiyo kukwama  hivyo klabu hiyo itaondoka nchini siku ya leo.

Kwa mujibu wa meneja na mratibu wa klabu ya Biashara United , Frank Wambare alisema kuwa, sasa wataondoka kesho (leo) Septemba 9, 2021 majira ya saa 10 jioni kupitia Uwanaj wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

‘’Tunatarajia kuondoka nchini  siku ya alhamisi 9 septemba kuelekea nchini Djibout majira ya saa10:00 jioni ili kuwahi mchezo wetu utakao chezwa siku ya ijumaa tarehe 10 septemba ‘’. Alisema Meneja

Klabu hiyo itaondoka na jumla ya wachezaji 30 pamoja na benchila ufundi na hakuna mchezaji yeyote alie ripotiwa kuwa majeruhi.

Biashara itakabiliana na klabu ya Dhikhil Fc katika hatua ya  awali ya kombe la shirikisho kwa kuanzia ugenini kisha itarejea kucheza itaikaribisha nyumbani timu hiyo baada ya wiki mbili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!