Wiki chache baada ya wanamgambo wa Taliban kuchukua madarakani na kuunda Serikali yao huko nchini Afghanistan, aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Ashraf Ghani ameibuka na kuwaomba msamaha raia wa Afghanistan baada ya kukimbilia nchi za Falme za Kiarabu. Na Mwandishi wetu… (Endelea)
Ghani aliondoka madarakani tarehe 15 Agosti, mwaka huu amesema aliondoka baada ya kushawishiwa na usalama wa Ikulu kwamba angeendelea kuwepo kungehatarisha maisha ya raia wengi.
Katika taarifa aliyoiweka kwenye mtandao wake wa Twitter amesema “Kuondoka Kabul ilikuwa moja ya uamuzi mgumu kuwahi kuufanya katika maisha yangu, lakini naamini hiyo ndio ilikuwa njia ya pekee kukwepa mtutu wa bunduki kutumika hivyo nikaamua kuokoa maisha ya watu milioni sita wanaoishi katika jiji la Kabul.
“Nimetumikia nchi hii kwa miaka 20. Katika maisha yangu nimeshirikiana na watu wa Afghanistan kujenga demokrasia, umoja na uzalendo. Sio lengo langu kabisa kuwaacha watu wangu na kuwatenga.
“Ninawaomba msamaha Waafghanistan wenzangu, sikutaka tumalize kwa tofauti zetu kwa kumwaga damu,” amesema.
Aidha, amesema katika maisha yake hakuwa kunuwia kujilimbikizia mali na kwamba taarifa zilizoibuliwa kuwa amekimbia na mamilioni ya Dola za Marekani katika nchi za Falme za kiarabu sio kweli.
Ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kwenda kukagua akaunti zake za benki kwani hata mkewe na familia yake anafahamu ukweli maisha ya kawaida wanaoishi.
Ghani mwenye umzi wa miaka 72, mwaka 2002 alihudumu kama waziri wa fedha chini ya utawala wa Rais Hamid Karzai, mwaka 2009 aliwania urais kwa mara ya kwanza na kushika nafasi ya nne kati ya wagombea wote.
Mwaka 2014 alifanikiwa kunyakua kiti hicho na kuhudumu kwa miaka mitano, kisha mwaka 2019 aliwania tena licha ya kutokea machafuko, duru ya pili ya uchaguzi ilipofanyika alishinda kisha akaapishwa tarehe 9 Machi 2020.
Aliondolewa madarakani tarehe 15 Agosti, mwaka huu baada ya wanamgambo wa Taliban kuvamia Ikulu na kuunda serikali yao
Leave a comment