December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Basi lateketeza maisha ya watu 50

Spread the love

BASI la abiria lililokuwa likitokea jijini Nairobi kuelekea Kisumu nchini Kenya, limepata ajali na kuua watu takribani 50. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ajali hiyo imetokea leo Jumatano alfajiri ya tarehe 10 Oktoba 2018, katika barabara ya Londiani-Muhuroni, Kaunti ya Kericho.

Basi lililopata ajali linamlikiwa na kampuni ya Western Express Sacco Limited.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Kericho, James Mogera amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kuongeza, “miongoni mwa waliokutwa na mauti, ni watoto nane walio chini ya umri wa miaka mitano.”

Amesema, majeruhi waliokuwa katika basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 67, wamepelekwa katika Zahanati ya Fort Ternan na Hospitali ya Kaunti ya Muhoroni Sub kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa basi kuvamia reli kisha kupanda katika shamba la mawe na kuanguka chini mita 20.

 

error: Content is protected !!