September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaonya madaktari

Dk. Faustin Ndungulile

Spread the love

MADAKTARI nchini wamepigwa marufuku kuandika dawa za wagonjwa kwa kutumia majina ya kampuni kwa kuwa kitendo hicho kinasababisha baadhi ya wagonjwa kukosa dawa.Anaripoti Mwandishi Wetu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 10 Oktoba 2018 na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Faustine Ndugulile, ambapo amesema kuwa, kitendo cha baadhi ya madaktari kuandika dawa kwa kutumia majina ya kampuni kinasababisha wagonjwa kushindwa kununua baadhi ya dawa zinazotengenezwa katika kampuni nyingine.

“Madaktari wawaandikie wagonjwa dawa kwa majina ya asili kwa sababu ukimwandikia mgonjwa panado ni kumtaka lazima anunue dawa hiyo hata kama kuna dawa nyingine hawezi kupewa,” ameeleza Dk. Ndugulile.

Dk. Ndugulile amewataka madaktari nchini kuwaandikia dawa wagonjwa kwa kutumia majina ya kitaalamu ili kuwawezesha wagonjwa kupata urahisi wa kununua dawa zenye uwezo wa kutibu maradhi yake.

error: Content is protected !!