July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vigogo wa vyama siasa wajifungia Dar kujadili Demokrasia

Viongozi wa Kisiasa na kidini wakiwa kwenye mkutano wa Amani na Utulivu ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere

Spread the love

BAADHI ya viongozi waandamizi wa vyama vya siasa hapa nchini leo tarehe 10 Oktoba 2018 wamekutana katika mkutano maalum unaoendelea kwenye hoteli ya New Afrika iliyoko jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Mkutano huo maalum kwa ajili ya kujadili kuhusu demokrasia hapa nchini, umeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kuwezeshwa na Taasisi ya Kujenga Azaki za kijamii Tanzania (FCSTZ).

Viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria katika mkutano huo ni pamoja na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Yeremia Maganja, pamoja na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CUF, Juma Duni Hajji.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini, kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa, mkutano huo ni mwanzo wa mjadala wa kitaifa kuhusu demokrasia kutokana na vyama vikuu vya siasa kutuma uwakilishi mkubwa.

“Mkutano Maalumu wa Viongozi wa vyama vya Siasa ulioandaliwa na @MwalimuNyerere Foundation na kuwezeshwa na @FCSTZ unaendelea hapa Hoteli ya New Afrika.Vyama vyote vikuu vimetuma uwakilishi mkubwa.Huu waweza kuwa mwanzo wa mjadala wa kitaifa kuhusu Demokrasia yetu @Twaweza_NiSisi,” ameandika Zitto.

error: Content is protected !!