Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Askari Polisi atwaa bodaboda ya NMB MastaBata
Habari Mchanganyiko

Askari Polisi atwaa bodaboda ya NMB MastaBata

Spread the love

ASKARI wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, WP Husna Juma Baraka, ameibuka mshindi wa pikipiki katika droo ya saba ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ inayoendeshwa na Benki ya NMB. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kampeni hiyi hadi sasa imeshatoa zawadi zenye thamani ya Sh 138 milioni kati ya zaidi ya Sh300 milioni zinazoshindaniwa.

 

Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Faraja Ng’ingo (kulia) akimkabidhi funguo ya Pikipiki mshindi wa droo ya sita ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’, Charles Shemsanga, kabla ya kuchezesha droo ya saba ya kampeni hiyo inayolenga kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu. Droo hiyo ilifanyika tawi la NMB Bank House jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Meneja wa tawi hilo, Lucas Malua. Katika droo hiyo Husna Juma Baraka wa Mtwara alijishindia Pikipiki, huku washindi 75 wakizawadiwa pesa taslimu Sh. 100,000 kila mmoja.

NMB MastaBata ni kampeni inayohamasisha matumizi ya kadi za NMB Mastercard na Lipa Mkononi (QR Code), badala ya pesa taslimu, ambako droo hiyo ilisimamiwa na Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kawili na kufanyika katika Tawi la Bank House.

Zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 300 zitatolewa kwa washindi 854 wa kampeni hiyo, wakiwemo 76 wa kila wiki, 51 wa kila mwezi na washindi saba wa ‘grand finale,’ ambako hadi kufikia jana, washindi walionufaika na MastaBata Kote Kote ni 587, wakijinyakulia zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 138.

Akizungumza kabla ya droo hiyo, iliyoambatana na makabidhiano ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya sita, Charles Shemsanga, Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Faraja Ng’ingo, alisema licha ya kuchagiza matumizi ya kadi, lakini pia wanaitumia MastaBata Kote Kote kurejesha kwa jamii sehemu ya faida yao.

Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Faraja Ng’ingo (katikati) akibonyeza kitufe cha kompyuta kuchezesha droo ya saba ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’, inayolenga kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu. Droo hiyo ilifanyika tawi la NMB Bank House jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kawili na kushoto ni Kaimu Meneja wa tawi hilo, Lucas Malua. Katika droo hiyo Husna Juma Baraka wa Mtwara alijishindia Pikipiki, huku washindi 75 wakizawadiwa pesa taslimu Sh. 100,000 kila mmoja

“Kupitia kampeni hii, tunawazawadia washindi 75 kila wiki kiasi cha Sh. 100,000 kila mmoja, huku mmoja akitwaa pikipiki, tunatoa pia pikipiki mbili kwa washindi wawili wa kila mwezi – sambamba na washindi 49 wa pesa taslimu Sh. Mil. 1 kila mmoja kwa droo za mwezi.

“Katika kuhitimisha kampeni hii, washindi saba (na wenza wao watakaowachagua) watajishindia safari ya Dubai iliyogharamiwa kila kitu na NMB, ambako watakaa kwa siku nne. Hii yote ni katika kuhamasisha matumizi ya kadi, ambayo kimsingi ni salama zaidi, nafuu zaidi kwa wateja wetu,” alisema Faraja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!