Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Mwaka 2022: Dk. Samia ameongoza kasi ukuaji mahusiano ya kidiplomasia na uchumi kati ya Tanzania, China
Makala & Uchambuzi

Mwaka 2022: Dk. Samia ameongoza kasi ukuaji mahusiano ya kidiplomasia na uchumi kati ya Tanzania, China

Spread the love

TUNAPOELEKEA kufunga mwaka 2022, ubalozi unatoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao uliowezesha utekelezaji wa Majukumu ya Ubalozi. Katika Mwaka 2022 mambo mbalimbali yenye tija na manufaa kwa wananchi yamefanyika kufuatia mwongozo na maelekezo ya Mwanadiplomasia namba moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyofanyika

Mosi; Tarehe 2-4 Novemba 2022 Ilifanyika ziara ya kihistoria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan-nchini China.  Kupitia ziara hiyo Tanzania na China zilipandisha hadi ya mahusiano kuwa ya Kimkakati katika nyanja zote.

Pili; Kwa upande wa biashara, mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la China yaliongezeka kutoka Dola za Kimarekani milioni 409 hadi kufikia Dola za Kimarekani milioni 605.5.  Inatarajiwa katika mwaka 2023 mauzo yataongezeka kwa asilimia 20 kutokana na Tanzania kufunguliwa soko jipya la bidhaa wakati wa ziara ya Rais Samia nchini China.

Tatu; Wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania wanaoshughulika na zao la parachichi walifunguliwa soko jipya la China mwezi Novemba 2022. Kuanzia msimo ujao wa 2023 mauzo ya parachichi katika soko la China yataanza.

Nne; Wavuvi wa Tanzania walifunguliwa soko jipya la kuuza mabondo ya samaki na samaki aina sangara nchini China mwezi Novemba 2022. Inatarajiwa mwaka 2023 mauzo ya bidhaa za uvuvi yataongezeka.

Tano; Bidhaa za Tanzania zilizoongezewa thamani zilianza kuuzwa katika soko la China kupitia mtandao maarufu wa Biashara wa JD.COM wenye watumiaji milioni 600- Mei 2022.

Sita; Watanzania walianza kufanya shughuli za usafirishaji wa mizigo yao moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China kwa kutumia Shirika la Ndege la Air Tanzania-  Mei 2022. Inatarajiwa mwaka 2023 baada ya China kufunguka shughuli zitaongezeka.

Saba; Usafiri wa abiria wa ndege wa moja kwa moja  kutoka Dar es Salaam hadi  Guangzhou ulianza Mwezi Julai 2022. Kuanzia Mwezi Januari 2023 wafanyabiashara,wanafunzi & watalii watanufaika na huduma hiyo baada ya hatua ya China kufungua mipaka na kuondoa masharti ya udhibiti wa UVIKO19

Nane; Kufuatia maelekezo ya Rais Samia, Ubalozi Mdogo wa Tanzania katika jijini la Biashara la China- Guangzhou ulifunguliwa rasmi mwezi Mei 2022.  Watanzania wameanza kupata huduma mbalimbali za kufanikisha shughuli zao za biashara na Ubalozi mdogo umeanza kufungua fursa mpya za masoko ya bidhaa.


Tisa; Filamu ya Tanzania Royal Tour ilioneshwa katika Televisheni ya Hainan Mwezi Oktoba 2022 na kutizamwa na watu milioni 60. Aidha, filamu hiyo iliyotafsiriwa kwa lugha ya kichina imeoneshwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ya China ikiwemo Bilibili m.bilibili.com/video/BV1jB4y1…

Kumi; Wanafunzi wa kitanzania watanufaika kwa kupata shahada na stashahada kufuatia kusainiwa kwa makubaliano mwezi Disemba 2022 kati ya Tasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),   na Taasisi ya Chongqing Vocation Institute of Engineering (CQVIE) ya China ya kuendesha mafunzo ya pamoja

11; Vijana wa kitanzania wataanza kunufaika na mafunzo ya ufundi kufuatia hatua ya ufunguzi rasmi wa Chuo cha Ufundi cha VETA mkoani Kagera kilichojengwa kwa msaada kutoka China na kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk @SuluhuSamia Mwezi Oktoba 2022.

12; Watanzania 122 wamepata ufadhili (scholarships) wa masomo ya Elimu ya Juu katika Vyuo Vikuu nchini China katika fani mbalimbali.  Mwaka 2023 watanzania wataendelea kupata fursa za masomo ikiwa ni sehemu ya matokeo ya ziara ya Rais Samia nchini China

13; Katika mwaka 2022 wafanyabiashara wa Tanzania wamepatiwa elimu kwa umma kuhusu fursa za biashara zilizopo nchini China pamoja na ushauri juu ya hatua za kuchukua ili kuepuka kuangukia mikononi mwa wafanyabiashara wasio waaminifu.

14; Katika mwaka 2022 vipindi vya elimu kwa umma vilianzishwa ili kuwapa wananchi ufahamu juu ya fursa za  upatikanaji wa teknolojia mbalimbali za bei nafuu kwa ajili ya uzalishaji/usindikaji wa malighafi zinazopatikana nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!