Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Michezo Mfalme wa Soka duniani – Pele afariki dunia
MichezoTangulizi

Mfalme wa Soka duniani – Pele afariki dunia

Spread the love

GWIJI wa soka raia wa Brazil – Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele amefariki dunia leo tarehe 29 Disemba, 2022 akiwa na umri wa miaka 82. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mchezaji huyo mashuhuri wa soka aliyeondoka kwenye umaskini wa kutembea bila ya viatu hadi kuwa mmoja wa wanasoka wakubwa na mashuhuri wanaojulikana sana katika historia, amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani.

Kifo cha mwanasoka huyo pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu akiwa mchezaji, kilithibitishwa na binti yake Kely Nascimento kwenye mtandao wa Instagram.

Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu 2021. Alikuwa amelazwa hospitali mwezi uliopita akiwa na maradhi mengi.

Aliibeba Brazil hadi kwenye kilele cha soka na kuwa balozi wa kimataifa wa mchezo huo katika safari iliyoanzia mitaa ya jimbo la Sao Paulo, ambapo alicheza mpira wa kutengenezwa na soksi iliyojaa magazeti au matambara.

Gwiji huyo wa Brazil, ambaye jina lake halisi lilikuwa Edson Arantes do Nascimento, aliisaidia nchi yake kushinda Kombe la Dunia mwaka wa 1958, 1962 na 1970 na anabakia kuwa kinara wa ufungaji wa timu ya taifa akiwa amefunga mabao 77 katika mechi 92.

Nyota wa sasa wa Brazil, Neymar, alifikisha magoli hayo kwenye Kombe la Dunia la mwaka huu nchini Qatar, akifunga bao lake la 77 katika michezo 124.

Pele alikuwa mfungaji mdogo zaidi wa Kombe la Dunia mwaka 1958 alipofunga bao dhidi ya Wales akiwa na umri wa miaka 17 tu mashindano hayo yalipofanyika Stockholm, Sweden.

Rekodi yake bado ipo, na hadi sasa, bado ndiye mchezaji pekee chini ya miaka 18 kufunga bao katika Kombe la Dunia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!