Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF yaitaka Serikali ije na mikakati kuondoa ukata kwa wananchi 2023
Habari za SiasaTangulizi

CUF yaitaka Serikali ije na mikakati kuondoa ukata kwa wananchi 2023

Spread the love

 

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeitaka Serikali ifikapo 2023 kuja na mkakati wa kitaifa wa kukuza uchumi, kuongeza ajira na kutoa huduma bora za kijamii kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akitoa tathimini ya 2022, leo Alhamisi tarehe 29 Desemba, 2022, jijini Dar es Salaam.

“Inatakiwa tuwe na mkakati wa kitaifa wa kukuza uchumi, kuongeza ajira na kutoa huduma muhimu kwa wananchi na haya yote yatafikiwa Kwa kuwa na siasa za kistaarabu, tushindane kwa sera na maamuzi ya wananchi kuchagua viongozi wao yaweza kuheshimiwa,” amesema Prof. Lipumba.

Mtaalamu huyo wa masuala ya uchumi, amesema Serikali inapaswa kuhakikisha Pato la taifa linakuwa Kwa asilimia nane kila mwaka ili kuendana na kasi ya ongezeko la watu nchini.

Katika hatua nyingine, Prof. Lipumba amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, asimamie upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025, Ili kuhakikisha chaguzi hizo zinakuwa huru na za haki.

“Tumemaliza 2022 kukiwa hakuna muelekeo wa mchakato wa kupata katiba mpya wala tume huru ya uchaguzi, tunavutiwa sana na kauli za Rais Samia na falsafa take ya maridhiano, kujenga umoja wa nchi na ustahimilivu, lakini kuna mambo naona hayajayatekeleza ikiwemo hayo,” amesema Prof. Lipumba.

Aidha, Prof. Lipumba amesema CUF inapongeza dhamira ya Serikali ya Rais Samia kuimarisha utawala bora na haki za binadamu, kwa kulifumua Jeshi la Polisi, kufuta kesi za kisiasa na na kubambikizwa ikiwemo ya ugaidi iliyokuwa inamkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Chadema, Freeman Mbowe na walinzi wake watatu.

Pia, Prof. Lipumba amesema CUF inapongeza juhudi za Rais Samia kuifungua nchi kiuchumi kitaifa na kimataifa huku akihimiza fedha za mikopo inayochukuliwa na Serikali zitumike kwa malengo kusudiwa ili kuleta maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!