Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mahakama yamhukumu mwandishi wa habari kifungo cha miezi 6
Habari Mchanganyiko

Mahakama yamhukumu mwandishi wa habari kifungo cha miezi 6

Spread the love

Mahakama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imemhukumu kifungo cha miezi sita jela mwandishi wa habari wa Congo, Stanis Bujakera baada ya kukutwa na hatia ya kueneza habari za uongo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wakili wa Bujakera, Jean-Marie Kabengela amesema jana Jumatatu majaji wametoa adhabu hiyo ya kifungo cha miezi sita pamoja na  kulipa faini ya faranga milioni 1 za Congo sawa na Sh 940,000.

Aliongeza kuwa Bujakera, ambaye anafanya kazi katika vyombo vya habari vya kimataifa ikiwa ni pamoja na Jeune Afrique na Reuters, anatarajiwa kuondoka katika gereza ambalo amekuwa akishikiliwa tangu Septemba mwaka jana kwa sababu tayari ameshatumikia muda huo.

Wakili huyo alisema, kwa kuzingatia taratibu za kawaida katika kesi hizo, timu ya mawakili inayomwakilisha Bujakera itarejea tena mahakamani hapo leo Jumanne, kupata nakala ya uamuzi huo na kulipa faini hiyo ili aachiliwe.

Bujakera, ambaye amekana mashtaka yote, alikamatwa katika mji mkuu Kinshasa kwa tuhuma za kueneza habari za uongo kuhusu mauaji ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani katika makala iliyochapishwa na Jeune Afrique, gazeti la habari la Ufaransa limesema.

Mwendesha mashtaka katika kesi hiyo mapema mwezi huu alikuwa ameitaka mahakama ya Kinshasa kumhukumu Bujakera kifungo cha miaka 20 jela.

Mashirika ya haki za ndani na kimataifa yakiwemo Reporters Without Borders na Amnesty International yalilaani kuzuiliwa kwa Bujakera, na kuliita shambulio dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11

Spread the loveKAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatarajiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

error: Content is protected !!