Friday , 10 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Kagame akubali kukutana na Tshisekedi
Kimataifa

Rais Kagame akubali kukutana na Tshisekedi

Spread the love

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Angola, Tete Antonio amesema jana Jumatatu jioni Rais Paul Kagame wa Rwanda amekubali kukutana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mazungumzo kuhusu hali ya usalama mkashariki ya Congo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Antonio amewaeleza hayo waandishi habari baada ya Rais Kagame kukutana na mwenyeji wake Joao Lourenco katika ikulu Lunda kwa mazungumzo juu ya ushirikiano kati ya nchi zao mbili.

Amesema katika mkutano huo walikubaliana kwamba Rais Kagame ataweza kukutana na Rais Tshisekedi katika wakati utakaofikiwa na wapatanishi.

Ofisi ya rais wa Rwanda kwenye ujumbe wake katika ukurasa wake wa X imeeleza kwamba wakuu hao wamekubali juu ya hatua muhimu kuelekea kutanzua sababu msingi wa ugomvi na haja ya kuheshimu utaratibu wa makubaliano ya Luanda na Nairobi wa kupatikana amani na utulivu katika ukanda mzima.

“Ujumbe wa Rwanda ulikubali kimsingi na ujumbe wa Congo kwamba mawaziri wao watafanya kazi pamoja ili kufikia lengo hilo,” amesema Antonio.

Mwishoni mwa mwezi Februari, Antonio amesema Rais Tshisekedi kimsingi ameshakubali kukutana na mwezake wa Rwanda. Mara ya mwisho viongozi hao kukutana ilikua tarehe 16 Februari kando ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa wakati wa mkutano mdogo wa kilele uliotayarishwa na Rais Lourenco.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!