Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Biashara Mikoa 30 yapata mikopo ya bil.324 kutoka SELF
Biashara

Mikoa 30 yapata mikopo ya bil.324 kutoka SELF

Spread the love

MFUKO wa Self umetoa mikopo ya zaidi ya Sh bilioni 324 kwa wananchi 314,055 wa mikoa 30 nchini huku ukijipanga kupanua wigo siku zijazo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Mfuko pia umesema katika mikopo iliyotoa kiwango cha mikopo chechefu ni chini ya asilimia 10, huku wakijipanga kukabiliana na changamoto ya mikopo kaushadamu.

Hayo yalisemwa jana Jumatatu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Mudith Cheyo akizungumza kwenye mkutano wa 53 wa ya taasisi hiyo na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam, kupitia uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Cheyo alisema hadi Desemba 31 mwaka jana, mfuko huo unaotarajia kuwezesha wananchi wengi kwa mikopo, ulifikia zaidi ya wananchi 300,000; wanawake 166,449 sawa na asilimia 53 na wanaume 147,606 sawa na asilimia 47.

Alisema pia umekopesha na kuzijengea uwezo taasisi ndogo 200 za fedha na kutengeneza ajira 37,024 kwa mwaka jana na kutoa elimu kwa wakopaji 1,519.

Ofisa Mtendaji huyo alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan, Mfuko wa Self umepata faida ya Sh bilioni 2 huku ikitoa gawio kwa serikali zaisdi ya shilingi milioni 240.

“Tumekuwa tukikua mwaka hadi mwaka, na tumepata faida ya Sh bilioni mbili, tukatoa gawio la zaidi ya Sh milioni 240, huku mtaji ukiongezeka kutoka Sh bilioni 56 hadi 62,” alisema.

Cheyo alisema mikakati yao ni ifikapo mwaka 2026 Mfuko uwe na matawi 20 kutoka 12 ya sasa, huku akisisitiza kuwa wamejipanga kuondoa mikopo kaushadamu.

Alisema kupitia mkakati wa kuongeza matawi wanatarajia kwa siku za karibuni watafikia kundi kubwa la Watanzania hasa kwenye SMEs ambao wanakadiriwa kufikia milioni nne.

Mkurugenzi wa Biashara wa Self, Petro Mataba alisema Mfuko unafanya kazi kwa kuzingatia uadilifu, ushirikiano, ubunifu, mteja na uwajibikaji, hali imewawezesha kukua kwa kasi.

Alisema Mfuko umetoa mikopo kwa wananchi na taasisi kama Kampuni ya Star Natural Product iliyokopeshwa Sh milioni 100 na shule ya Bright Future Academy Sh milioni 400.

Alitaja changamoto zilizopo kuwa ni wananchi wengi kukosa elimu ya fedha, kujishughulisha na biashara zisizo rasmi na kukosa utamaduni wa kukopa na kurejesha, ingawa wanaendelea kutoa elimu ili wabadilike.

Mkurugenzi wa Masoko, Santiel Yona alisema mpango mkakati wao ni kufikia wateja wengi hasa wa kipato cha chini, kuongeza ufanisi na kuhakikisha taasisi inakuwa endelevu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

error: Content is protected !!