Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aonya taasisi, mashirika ya umma yanayokopa kutoa gawio
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia aonya taasisi, mashirika ya umma yanayokopa kutoa gawio

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema anataka kuona taasisi na mashirika ya umma yakichangia mfuko mkuu wa serikali kutokana na kipato kinachozalishwa kwa kutekeleza majukumu yao na sio kwenda kukopa ili kutoa gawio kwa Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema anatambua kuwa kuna mashirika hayachangii chochote hadi sasa kwenye mfuko huo wa serikali kutokana na hali halisi ya mashirika hayo.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Agosti 2023 wakati akifungua kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wa mashirika ya umma kinachofanyika jijini Arusha.

“Wakati tulipolazimishwa kila shirika lazima litoe gawio natambua kwamba wakati ule unakuwa wakati mgumu kweli kwa Ma-CEO na bodi zao hadi wanaamua kwenda kukopa ilimradi tu wapeleke gawio kunusuru nafasi zao…  sasa kwa kuijua hali ile nikasema hapana.

“Wanaofanya faida walete gawio, wasiofanya faida tuwaangalie kwanini hawafanyi faida, kuna changamoto zipi na vikwazo vipi na tuwasaidie watoke huko waende wakazalishe walete faida hicho ndio tunachokwenda kufanya sasa,” amesema.

Aidha, amesema kutokana na mageuzi yanayokwenda kufanywa kwenye mashirika hayo, watendaji na wenyeviti wa bodi wajitafakari na kila mmoja aende akasimame kwenye nafasi yake sawasawa kwani mageuzi hayo ni ya lazima ili mashirika hayo yajiendeshe na serikali ipate faida.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!