IDADI ya raia walio na umri wa zaidi ya miaka 60 nchini China inatarajiwa kuongezeka kwa wastani wa milioni 10 ifakapo mwaka 2050 ambapo inatarajiwa kutakuwa na wazee milioni 520. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Inaelezwa kuwa suala hili limeongeza wasiwasi kwa mamlaka kuhusu hazina ya serikali ya pensheni, vituo vya kulelea wazee na huduma za matibabu.
Makamu wa Rais wa Chuo kikuu Renmin cha China Du Peng ameeleza ididai hiyo ni sawa na asilimia 37.8 ya watu wote nchini humo.
China ilikuwa na watu milioni 209.78 wenye umri wa zaidi ya miaka 65 mwaka jana, ikiwa ni asilimia 14.9 ya watu kwa mwaka 2021.
Du alipohojiwa na Tencent Finance alieleza kuwa sasa ni wakati wa China kujiandaa kikamilifu kukakabidili idadi kubwa ya wazee.
Leave a comment