Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kanisa Katoliki ‘lashusha kombora’ DP World
Habari MchanganyikoTangulizi

Kanisa Katoliki ‘lashusha kombora’ DP World

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tazania (TEC), Padri Charles Kitima
Spread the love

 

BARAZA la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC), limepinga mkataba wa usimamizi na uendelezaji wa bandari nchini, kati ya Tanzania na kampuni ya kigeni ya DP World ya Dubai. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Tamko la baraza hilo, lililoridhiwa na Maaskofu 37 wa Kanisa Katoliki nchini linasema, Baraza hilo haliungi mkono mkataba wa uwekezaji wa bandari, kwa kuwa umesheheni vifungu vinavyonya wananchi.

Tamko la maaskofu Katoliki limetangazwa kwa umma na katibu mkuu wa TEC, Padre Dk. Charles Kitima.

Limetolewa takribani siku 40 baada ya Bunge la Jamhuri, kuridhia Mkataba wa Ushirikiano kati ya Dubai na Tanzania.

Dk. Kitima amesema, maaskofu hawaungi mkono bandari kuwekwa chini ya mwekezaji mmoja na kwamba tamko hilo la maaskofu lina lugha moja tu, nayo ni kwamba “kama wananchi hawautaki mkataba, serikali iwasikilize wananchi wake.”

Kanisa Katoliki linasema, “tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe.

“Kwa kuwa tumeonyesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; ni wajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe, huku tukikaribisha ubia tunaodhibiti wenyewe.

“Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile, tumegundua mapungufu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu.

“Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, hatuungi mkono mkataba huu. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.”

Tamko la TEC, limeanza na neno: “Sauti ya Watu, Sauti ya Mungu.”

1 Comment

  • Ratiba ya Ziara ya Mary Pius Chatanda KIONGOZI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) KWENYE SEKTA YA MADINI ATATEMBELEA:-
    • Mgodi wa Dhahabu
    • Mgodi wa Almas(Kampuni ya Petra Diamond Ltd)
    • Mgodi wa Gas
    • Mgodi wa Uranium
    • Mgodi wa Mafuta
    • Mgodi wa Makaa ya mawe
    • Mgodi wa Tanzanite
    • Mgodi wa Uchimbaji Madini na Mawe
    • Ujenzi wa vituo vitatu vya umahiri
    • Masoko ya madini
    • Kampuni ya Mahenge Resources Limited (Black Rock Mining Ltd)
    Kuanzia tarehe 23/8/2023 hadi tarehe 2/8/2023v

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

error: Content is protected !!