Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Slaa: Sitarudi nyuma, nimetimiza wajibu wangu
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Sitarudi nyuma, nimetimiza wajibu wangu

Spread the love

 

BALOZI Dk. Willibroad Slaa leo Ijumaa amesema kitendo cha polisi kumkamata kinguvu tarehe 13 Agosti 2023 kisha kutuhumiwa kwa uhaini, hakitamrejesha nyuma katika jitihada zake za kutetea rasilimali za Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam baada ya kuachiwa kwa dhamana amesema; “Wasifikirie kitendo cha kunichukua siki ile kwa nguvu kama kitanirejesha nyuma kushiriki na watanzania wenzangu kujadili rasilimali zetu sitarudi nyuma.

“Ninachojua nimetimiza wajibu wangu wa kikatiba ya kupiga kelele juu ya rasilimali kama ni kosa basi hatuna Katiba itakuwa ni karatasi tu…sitashaanga Katiba hii kuvunjwa kwani imekuwa ikivunjwa kila siku,” amesema na kuongeza;

“Kama Bunge halisemi haya sisi tutayasemea …kama wabunge tuliowachagua hawatekelezi wajibu wao hata wakituita wachochezi kama kutuweka jela watuweke tu. Afadhali uhukumiwe duniani kuliko kuhukumiwa mbinguni.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!