Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Slaa aionya Serikali marekebisho sheria ya rasilimali asilia
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa aionya Serikali marekebisho sheria ya rasilimali asilia

Spread the love

 

BALOZI Dk. Willibroad Slaa amedai kuwa katika Mkutano wa 12 wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 29 Agosti 2023, iwapo marekebisho ya muswada wa sheria ya rasilimali asilia yatapita masuala yote yanayohusu rasilimali za nchi yataanza kujadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri na si bungeni tena. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ametaja baadhi ya vifungu vya muswada huo ambao unakwenda kufanyiwa marekebisho kuwa kifungu cha 38 (2) (a) na (b) hatua ambayo inakwenda kuangamiza Taifa kama marekebisho hayo yatapita.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake leo Ijumaa Jijini Dar es Salaam baada ya kuachiwa kwa dhamana, Dk. Slaa amesema muswada huo utakaowasilishwa bungeni, uliwasilishwa bungeni kwa hati ya dharura Juni mwaka huu ikiwa ni baada ya kuchapishwa tarehe 10 Mei, 2023.

Amesema sheria inayohusiana na rasilimali asilia inaipa Tanzania uhalali wa kumiliki rasilimali na hadhi ya kuwa nchi huru ambayo inamiliki rasilimali zake.

“Mambo mazito yanayohusu Watanzania, yanaondolewa sasa bungeni yanapelekwa kwa baraza la mawaziri, naomba niwaonye vitu viwili katiba yetu inasema baraza la mawaziri ni chombo cha ushauri sio lazima Rais apokee ushauri wao.

“Pili tangu uhuru masuala yanayojadiliwa na baraza la mawaziri pamoja ya kuwa ni ushauri hayawezi kujadiliwa popote ikiwemo mahakamani kwani huwezi kuhoji maamuzi ya baraza la mawaziri mahakamani… muone Taifa linarudi kwenye giza labda karne ya 15, tunarejea kwenye giza badala ya kupiga hatua mbele sisi tunapiga hatua 10 nyuma katika mambo ya demokrasia,” amesem Dk. Slaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!