Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Slaa aachiwa kwa dhamana, Mwabukusi, Mdude kitendawili
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa aachiwa kwa dhamana, Mwabukusi, Mdude kitendawili

Spread the love

HATIMAYE Balozi Dk. Wilbroad Slaa leo Ijumaa mchana ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana aliyoagizwa na Jeshi la Polisi Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu ..(endelea).

Wakili wa mwanasiasa huyo mkongwe, Dickson Matata amethibitisha kuachiwa kwa Dk. Slaa katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam baada ya jana usiku kurejeshwa jijini hapa kutokea mkoani Mbeya.

Awali Wakili Matata aliueleza MwanaHALISI Online kwamba polisi walimpigia simu na kumtaka afike kituoni hapo kukamilisha taratobu za dhamana ya mteja wake.

“Polisi wametaka wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kata wanazoishi,” amesema.

Dk. Slaa alikamatwa Jumapili iliyopita nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za uchochezi na uhaini ambazo pia watuhumiwa wengine Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali wanakabiliwa nazo.

Hata hivyo, wote walisafirishwa kupelekwa Mbeya kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka hayo lakini sasa Dk. Slaa jana amerejeshwa Dar es Salaam na kuachiwa kwa dhamana huku hatima ya  watuhumiwa wenzake ikiwa haifahamiki.

Watuhumiwa hao walikmatawa baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillius Wambura wiki iliyopita kuueleza umma kuwa kuna watu wamepanga maandamano yasiyo na kikomo na kutaka kuipindua Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!