Friday , 10 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee ang’ang’ania mshahara wa waziri kisa madai ya watumishi
Habari za Siasa

Mdee ang’ang’ania mshahara wa waziri kisa madai ya watumishi

Halima Mdee
Spread the love

 

MBUNGE Viti Maalum, Halima Mdee (Chadema), ametishia kutopitisha fungu lenye bajeti ya mashahara wa Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, endapo hatatoa majibu ya kuridhisha kuhusu muarobaini wa madai ya watumishi wa umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tukio hilo limetokea leo tarehe 20 Aprili 2023, bungeni jijini Dodoma, wakati wabunge wanapitisha mafungu ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa 2023/24.

Mdee alisema atashika shilingi katika fungu namba 32 ambalo lina mshahara wa waziri wa wizara hiyo.

Mdee amedai kuwa, taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika nyakati tofauti zinaonyesha malimbikizo ya madai ya watumishi yanakuwa kwa kasi, licha ya hatua inayochukuliwa na Serikali kuyalipa.

“Taarifa zimekuwa zikionyesha madai ya watumishi yamekuwa yakikuwa kwa kiwango kikubwa na madai ya waziri yamejikita kwenye mishara.

“Taarifa za CAG zimekuwa zikionyesha mfano 2020/21 madai ya watumishi yalikuwa Sh. 429 bilioni na sasa inakadiriwa kuwa Sh. 509 bilioni. Changamoto hii imekuwa kubwa kutokana na ucheleweshaji,” amesema Mdee.

Mdee amesema “tunaenda kinyume na kanuni na wacheleweshaji wakubwa ni wizara ya fedha. Nataka nipate majibu yenye tija sababu juhudi za Rais zinaonekana kupunguza lakini haziondoi. Nataka majibu, yasiporidhisha nakamata shilingi.”

Kufuatia hoja hiyo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, alitoa ufafanuzi akisema Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Serikali yake wanaendelea kulipa malimbikizo ya madai ya watumishi.

Hata hivyo, wabunge hao walipitisha bajeti ya wizara hiyo ya Sh trilioni 1.1 ambayo iliwasilishwa bungeni jana na Simbachawene.

1 Comment

  • Duh!
    Siyo ucheleweshaji. Ni wivu tu! Yaani kijana anamuonea wivu mstaafu wa miaka 60 anapotaka kuchukua haki yake ya kibunda chake! Acheni tabia hii ya wivu.
    Sheria itungwe na si kulalamika tu!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Spread the loveMBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

error: Content is protected !!