Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Mwinyi ataja mikakati kushusha bei ya mafuta Zanzibar
Habari Mchanganyiko

Rais Mwinyi ataja mikakati kushusha bei ya mafuta Zanzibar

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi , amesema Serikali yake inakusudia kuboresha miundombinu ya bandari pamoja na hifadhi ya kutosha ya mafuta, ili kushusha bei yake inayotokana na kuhifadhiwa nje ya visiwa hivyo. Anaripoti Mwandishi Wetyu, Zanzibar … (endelea).

Rais Mwinyi ametoa taarifa hiyo leo tarehe 4 Machi 2023, akizindua Bohari ya Mafuta katika Bandari ya Mangapwani, visiwani Zanzibar.

Amesema uboreshwaji wa maeneo hayo utapelekea mafuta kusafirishwa moja kwa moja kutoka sokoni hadi Zanzibar, kitendo kitakachopunguza gharama za uhifadhi na usafirishaji.

“Kwa hali ya sasa Zanzibar hatuleti mafuta moja kwa moja, yakitoka Dar es Salaam yanahifadhiwa Tanga sababu hapa hatuna hifadhi ya kutosha, yakitoka Tanga yanaletwa Zanzibar. Haya yote yanasababisha mafuta kuwa na bei hii,” amesema Rais Mwinyi na kuongeza:

“ Nini tunataka kufanya, tukishakuwa na hifadhi ya kutosha na gati ya kutosha, meli moja kwa moja itashusha Zanzibar, tutakuwa na mafuta bei rahisi. Na huo ndiyo mpango na azma ya Serikali, tutafanya kila linalowezekana hilo litimie na maslahi ya nchi kwenda mbele.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!