Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yavuna wanachama wa CUF, CCM, Chadema Zanzibar
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yavuna wanachama wa CUF, CCM, Chadema Zanzibar

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeendelea kuvuna wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) baada ya kuwapokea 305 kupitia mkutano wake wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Tibirinzi, kisiwani Pemba, Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, wanachama hao wamejiunga na chama hicho leo tarehe 4 Machi 2023, katika mkutano huo uliofanyika visiwani Zanzibar.

Mbali na wanachama hao wa CUF, taarifa ya Shaibu imesema ACT-Wazalendo imepokea wanachama 10 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mmoja kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kupitia taarifa hiyo, Shaibu amesema kundi la wanachama hao liliongozwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF Zanzibar, Abbas Juma Muhunzi.

“Chama cha ACT Wazalendo, kwenye Mkutano wake Kisiwani Pemba uliofanyika katika viwanja vya Tibirinzi leo tarehe 04 Feb kimewapokea wanachama 305 wa CUF, 10 wa CCM na mmoja wa Chadema wakiongozwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF Zanzibar Ndugu Abbas Juma Muhunzi,” imesema taarifa ya Shaibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!