Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais samia apiga ‘stop’ viongozi kuamua kwa maagizo kutoka juu
Habari za Siasa

Rais samia apiga ‘stop’ viongozi kuamua kwa maagizo kutoka juu

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi na watendaji wa Serikali, kuacha kufanya maamuzi kwa kisingizio cha maagizo kutoka juu, bali kwa kufuata sheria na kuwa tayari kutetea maamuzi yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo tarehe 4 Machi 2023, akifunga mkutano wa faragha wa mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu, uliofanyika jijini Arusha.

“Nendeni mkafanye kazi kwa kujiamini, mnapofanya maamuzi sema haya ni maamuzi yangu na nimeamua haya kutokana na moja mbili tatu, sheria inasema moja mbili tatu. Tusielekee kule mbona umeamua hivi aaah ni maelekezo kutoka juu. Hapana, utakuwa hujiamini naomba sana tukajiamini fanya maamuzi kwa kujiamini na uwe tayari kusimama kutetea maamuzi yako,” amesema Rais Samia.

Wakati huo huo, Rais Samia amewataka viongozi wa Serikali kuacha kuwadharau wananchi kwa kuwa ndiyo wenye nchi hivyo wanapaswa kuheshimiwa.

“Twende tukaache migongano, kusengenyana na tukaaminiane tuache kuhujumiana na uzembe ili twende tukafanye kazi za watu. Kubwa zaidi tuache dharau pia, tunaowahudumia ni wananchi wenye nchi hii, kwa hiyo hawafai kudharauliwa. Wala tusidharauliane sisi wenyewe kwa wenyewe, twendeni tukafanye kazi kwenye misingi ambayo tumekumbushwa,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, amewataka viongozi hao kutanguliza mbele maslahi ya taifa wakati wanapotekeleza majumuku yao ya kila siku, pamoja na kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!