Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi 716,664 kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni hadi sasa
Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 716,664 kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni hadi sasa

Wanafunzi
Spread the love

IKIWA ni wiki moja tangu kufunguliwa shule nchini Tanzania jumla ya wanafunzi 716,664 wanaopasa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023 bado hawajaripoti na kuandikishwa sawa na asilimia 67. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumapili tarehe 15 Januari, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msingwa, wanafunzi 354,277 wakiwemo wenye ulemavu 697, ndiyo waliojiandikisha hadi sasa kati ya wanafunzi 1,070,941 wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza sawa na asilimia 33 ya matarajio.

Aidha amesema watoto walioandiskishwa kwa aajili ya kuanza darasa la kwanza ni 1,446,067 wakiwemo wenye ulemavu 2,942 saw ana asiliia 88.48 ya matarajio ya kuandikisha watoto 1,634,365.

Msigwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kwenda sekondari wanaripoti shuleni.

Amesema Serikali inagharamia elimu ya msingi na Sekondari kwa kutoa Sh 29 bilioni kila mwezi sambamba na kutoa maelekezo mahususi juu ya michango kwa wanafunzi wanaoingia shuleni lengo likiwa ni kuondoa vikwazo vya wanafunzi kujiunga na shule.

Vilevile amesema jumlanya wanafunzi 14,581 wameandikishwa katika Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) na kati ya hao 334 ni wenye mahitaji maalum.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!