HADI kufikia tarehe 09 Januari, 2023 wakulima 560,451 wamenufaika na mbolea ya ruzuku sawa na asilimia 20 ya wakulima 3,264,440 waliosajiliwa kupata mbolea nchi nzima. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Wakulima hao hadi sasa wamesambaziwa mbolea ya ruzuku tani 194,259 yenye thamani ya Sh 208.6 Bilioni.
Akizungumz ana waandishi wa habari leo Jumapili tarehe 15 Januari, 2023, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema zoezi la usambazaji linaendelea.
“Na hivi sasa kwa wale wakulima wenzangu na mimi huu ndio muda wa mbolea za kukuzia baada ya wengi kuwa wamekamilisha kupanda kwani kalenda ya kilimo inaelekeza kuwa tarehe 15 ndio mwisho wa kupanda zao la mahindi,” amesema Msigwa.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeongeza bajeti ya kilimo kutoka Sh 254 Bilioni mwaka 2021/22 hadi Sh.954 bilioni na kutoa ruzuku ya Sh 150 Bilioni kwa ajili ya kupunguza mfumuko wa bei ya mbolea nchini.
Ruzuku hiyo imepunguza nusu ya bei ya awali ya mbolea ambapo mfuko wa kilo 50 ulikuwa unauzwa Sh 150,000 ulishuka hadi Sh 75,000.
Leave a comment