SERIKALI nchini Tanzania imesema mwaka huu imeanza rasmi utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya msingi na awali (BOOST) utakaogharimu Sh. 1.15 trilioni kwa kipindi cha miaka mitano. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Mradi huo utaangazia zaidi miundombinu ya shule za msingi na awali na umeanza mwaka 2022/2023 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2026/2027.
Hayo yameelezwa leo Jumapili tarehe 15 Januari, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msingwa katika taarifa yake mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma.
“Naa hivi sasa tunakuja na kishindo kingine kikubwa. Tunao mradi mwingine mkubwa wa kuboresha elimu ya awali na msingi unaoitwa BOOST. Kwenye eneo hili tunataka kupeleka nguvu nyingi kukabiliana na miundombinu ya shule za msingi na awali ili watopto wetu wasome sehemu nzuri,” amesema Msigwa.
Amesema kwa kuanzia katika mwaka huu 2023 Serikaoi imepanga kutumia Sh. 250 bilioni ambazo zitajenga madarasa 900 kwaajili ya shule za msimngi na awali.
“Naombeni ndugu zangu waandishi wa habari twendeni kwenye shule ambazo madarasa haya yamejengwa tupige picha na truoneshe wananchi kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita,” amesema.
Leave a comment