Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa BAVICHA kuongoza vijana wa vyama vya demokrasia Afrika
Habari za Siasa

BAVICHA kuongoza vijana wa vyama vya demokrasia Afrika

Spread the love

BARAZA la Vijana la Chama cha Chadema (BAVICHA), litaongoza Umoja wa Vijana wa Afrika kutoka vyama vya kidemokrasia (YDUA), katika kipindi cha mwaka mmoja (2022-2023), kupitia mjumbe wake Gwamaka Mbugi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ni baada ya Mbugi aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa YDUA, kuteuliwa kuwa Mwenyekiti akishika nafasi ya Louisa Atta-Agyewang, aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Afrika (DUA).

Akizungumza na wanahabari jana tarehe 26 Novemba 2022, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano BAVICHA, Apolinary Boniface, amesema hatua hiyo ni fursa kwa vijana wa Chadema na taifa kwa ujumla.

“Bavicha tunajivunia kuongoza taasisi kubwa hii vijana Afrika, ambayo itakuwa fursa kubwa chama, vijana na taifa kwa ujumla.Tunampongeza na kumtakia heri Gwamaka Mbugi katika kuongoza taasisi hiyo muhimu kwa vijana. Bavicha tutaitumia fursa hiyo kusukuma agenda za vijana,” amesema Boniface.

Boniface amesema kuwa siyo mara ya kwanza kwa Bavicha kuongoza nafasi za kimataifa.

“Bavicha tunaongoza nafasi zingine kimataifa, Dorcas Francis kutoka Bavicha ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Vyama vya kidemokrasia Duniani (IYDU). Pia Hellen Sisya ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Umoja wa Vijana wa Vyama vya Kidemokrasia Afrika (YDUA).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!