Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Tulia: UVCCM msikae kimya
Habari za Siasa

Spika Tulia: UVCCM msikae kimya

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson, ameutaka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), usikae kimya katika kuwaeleza wananchi maendeleo yanayofanywa na Serikali, kwani kitendo hicho kitawalinda viongozi walioko madarakani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Spika Tulia ametoa wito huo leo tarehe 26 Novemba 2022, akizungumza katika matembezi ya UVCCM yaliyofanyika jijini Dodoma.

“Niwaombe sana kuja kwetu hapa kuwe ni chachu ya hamasa, mrejeapo kwenye mikoa yenu mkaendeleze mazoezi kusema kazi nzuri zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, mkaendelee kueleza kazi nzuri zinazofanywa na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi. Msikae kimya waelezeni wananchi,” amesema Spika Tulia.

Aidha, Spika Tulia amewataka vijana wa UVCCM kuwa wa kwanza kuanzisha hoja, badala ya kusubiri wengine kutoka vyama vya upinzani kuanzisha masuala aliyoyaita kuwa ni vioja.

“Tusisubiri wenzetu waanzishe vioja halafu ndiyo tufanye kazi ya kuwajibu, anzisha wewe hoja wakibisha wape data. Sisi sio watu wa kuanzishiwa vioja halafu tuanze kubisha, sisi kazi yetu kuanzisha hoja, walete vioja tuwape hoja,” amesema Spika Tulia.

Spika Tulia amewataka vijana wa CCM kueleza miradi ya maendeleo inayotoekelezwa na Serikali katika maeneo yao ili wananchi wapate kuelewa kazi inayofanywa na viongozi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!