Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Tanzania kuandaa mpango kuhakikisha inashiriki Kombe la Dunia 2030
Michezo

Tanzania kuandaa mpango kuhakikisha inashiriki Kombe la Dunia 2030

Spread the love

 

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa amesema Wizara hiyo inaandaa mpango mkakakati kuhakikisha 2030 Tanzania inashiriki kombe la Dunia, huku akiweka bayana kuwa hawatavumilia mtendaji yoyote ambaye atawakwamisha. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea),

Mchengerwa aliyasema hayo jana Alhamisi tarehe 27, Oktoba, 2022, wakati akizindua Program ya Mpira Fursa na kutoa vifaa vya michezo kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (FDC) 54, vilivyotolewa na Shirika la Karibu Tanzania (KTO).

Alisema KTO imeonesha mfano sahihi katika kukuza soka la wanawake, hivyo ni jukumu la watendaji wakuu wa wizara hiyo kuhakikisha juhudi hizo zinaungwa mkono, ili mpango mkakati wa kushiriki kombe la dunia 2030 inatimia.

Mimi, naibu waziri, katibu mkuu na naibu katibu mkuu tumeshakubaliana kuwa katika wizara hii hakuna jambo la kutushinda, jambo lolote linalokuja lazima tulishinde, tumekuja na mkakati wa kutupeleka kombe la dunia 2030, tupo tayari kupokea mapendekezo yoyote ya kuhakikisha tunafikia huko.

“Mmesema mnamtaka Ally Mayayi aoneshe yale ambayo anayazungumzia Azam TV, huyu hapa, sasa atuoneshe uwezo wake kwa kushirikiana na wenzake watuambie tufanyeje ili kupiga hatua, tupo tayari kuwapa sapoti yote kufanikisha mkakati wetu wa miaka nane unatimia, akishindwa tunamuondoa,” alisema.

Alisema haingii akilini kuona wakina mama wanafanya vizuri lakini wanaume hawafanyi vizuri, hivyo ni lazima kubadilika na hoja ya viwanja isitumiwe.

Waziri Mchengerwa alisema KTO wameanza kutafsiri neno mtaa kwa mtaa, hivyo nasisitiza kila mtaa ucheze mpira kama ambavyo dhamira ya Mpira Fursa inavyotaka katika kukuza mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake.

Alisema wizara imedhamiria kupokea kila kijana ambaye ana kipaji cha michezo na kumtumia na ifikapo 2030 Tanzania iwe kijiji cha michezo.

Mchengerwa amewataka KTO kuendeleza program hiyo katika ngazi ya shule za sekondari, vyuoni na upande wa Zanzibar ili tafsiri sahihi ya muungano iweze kutimia.

“Hawa KTO wameonesha njia naomba wadau wengine kuungano nao, sisi Serikali tutatoa ushirikiano kuhakikisha michezo inafanyika kila kona ya nchi,” alisema.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo, Mratibu wa Mpira Fursa Miya Mjengwa alisema KTO imeamua kuja na fursa hiyo ili kuweza kuibua vipaji vya vijana wa kike ambao wapo mitaani, ili waweze kupata ajira.

Alisema tangu programa hiyo pia wanawake na wasichana wanajifunza ufundi seremala na stadi za maisha kwa ujumla, hali ambayo inawahakikishia ajira zinazowaingizia kipato.

Miya alisema program hiyo imewezesha kupata makocha wanawake 54 katika vyuo vya maeaneleo ya jamii 54, ambapo wengine wanatumia na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) katika baadhi ya michezo.

“Sisi tunataka mpira uchezwe kila kona, hivyo kupitia FDC tunatarajia kufikia vijana na wakina mama zaidi 10,000 kwa siku za karibuni, hali ambayo itatimiza lengo letu la kumkomboa mtoto wa kike,” alisema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!