Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko   Uwekezaji Kidijitali – NMB yaendelea kukuza Uchumi wa Buluu
Habari Mchanganyiko

  Uwekezaji Kidijitali – NMB yaendelea kukuza Uchumi wa Buluu

Spread the love

BENKI ya NMB imekuwa mstari wa mbele kwa ubunifu katika sekta ya TEHAMA kwa kutoa masuluhisho mbalimbali kwa wateja wake wa nyanja zote.

Sehemu ya wadau na washiriki wa Kongamano la sita la TEHAMA (Tanzania Annual ICT Conference) wakifuatilia wasilisho la Benki ya NMB

NMB wameshiriki katika Kongamano la sita la TEHAMA (Tanzania Annual ICT Conference) linalofanyika kwa mara ya kwanza Visiwani Zanzibar na kuzinduliwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

 

Mkaguzi wa Ndani wa NMB – Benedicto Baragomwa (pili kushoto), akishiriki mjadala wakati wa Kongamano la sita la TEHAMA (Tanzania Annual ICT Conference) linaloendelea Visiwani Zanzibar.

Kauli mbiu ya kongamano hilo ni Mabadiliko ya Kidijitali kwenye Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi.

Akifanya wasilisho la benki hiyo, Mkaguzi wa Ndani wa NMB – Benedicto Baragomwa alisema kuwa, wametumia fursa ya kongamano hili lenye zaidi ya washiki zaidi ya 800 wakiwemo viongozi wa serikali, watalaam wa TEHAMA, wadau wa maendeleo pamoja na wawekezaji katika sekta ya TEHAMA kutoka ndani na nje ya nchi kuonyesha uwezo, utayari na ushiriki wao katika kuwawezesha wananchi kutumia fursa zinazotokana na uchumi wa buluu.

Aidha, NMB imekuwa mchangiaji Mkuu wa ukuaji wa Uchumi wa Buluu Zanzibar kupitia makubaliano mbalimbali iliyosaini kuleta mabadiliko ya teknolojia ikiwemo; ushirikiano wao na Umoja wa Kampuni za Kutoa Huduma za Utalii Zanzibar (ZATO) uliozaa Kadi Maalum ya Malipo Kabla (NMB, ZATO Prepaid Card) na ule wa Wakala wa Serikali Mtandao (NMB e’Government Zanzibar) kushirikiana na NMB kutengeneza mfumo jumuishi (One Stop Center System) utakaotumika na taasisi Taasisi za SMZ.

Mkaguzi wa Ndani wa NMB – Benedicto Baragomwa akitoa wasilisho la NMB, kwa wadau wa Kongamano la sita la TEHAMA (Tanzania Annual ICT Conference) linalofanyika kwa mara ya kwanza Visiwani Zanzibar. Kongamano hilo limeanza Oktoba 26 hadi 28, 2022.

“Kupitia NMB e’Government Zanzibar, benki imewezesha ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Malipo Kidijitali ‘One Stop Center’ cha Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC), ambako malipo mbalimbali pale hupitia ‘control number’ moja na hivyo kurahisisha makusanyo na kukuza pato la Serikali inayochakata sera ya Uchumi wa Buluu,” alifafanua Baragomwa.

Lakini pia katika ‘Uchumi wa Buluu’ NMB wamepunguza matumizi ya pesa taslimu ‘cashless’ kupitia hiyo ‘one stop center’ na PoS,na hivi karibuni wamezindua mashine ya ATM ya kubadili fedha za kigeni kama paundi, dola na euro kuwa shilingi za Kitanzania kwa saa 24  katika uwanja wa ndege wa Amani Abeid Karume.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *